Kiongozi Muadhamu: Uhusiano wa Iran na Korea Kusini lazima uendelee
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i6283-kiongozi_muadhamu_uhusiano_wa_iran_na_korea_kusini_lazima_uendelee
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesisitizia umuhimu wa kuendelezwa uhusiano imara na usioweza kuathiriwa na vikwazo na uhasama wa Marekani baina ya Iran na Korea Kusini,.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 03, 2016 00:00 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Uhusiano wa Iran na Korea Kusini lazima uendelee

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesisitizia umuhimu wa kuendelezwa uhusiano imara na usioweza kuathiriwa na vikwazo na uhasama wa Marekani baina ya Iran na Korea Kusini,.

Ayatullah Ali Khamenei aliyasema hayo jana jioni alipokutana na Rais Park Geun-hye wa Korea Kusini ambapo sanjari na kuashiria mtazamo chanya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran juu ya umuhimu wa kuongezwa uhusiano na nchi za Asia alitaja kuendelezwa uhusiano baina ya Tehran na Seoul ambao utakuwa imara na kutoathiriwa na vikwazo na uhasama wa Marekani, kuwa ni jambo lenye manufaa. Akifafanua suala hilo Kiongozi Muadhamu alisema kuwa, maelewano na mikataba baina ya Iran na Korea Kusini lazima iimarishwe kiasi cha kuzuia vizingiti vya nje na vikwazo kutoweza kuwa na athari hasi juu yake kwani ni jambo lisilofaa kuona mahusiano ya nchi mbili hizi yakiathiriwa kwa aina yoyote na Marekani. Akiashiria hatua ya Marekani kuugawa ugaidi katika makundi mawili ya ugaidi mzuri na mbaya amesema kuwa, Marekani imekuwa ikitoa nara za kupambana na ugaidi katika hali ambayo kivitendo haina ukweli kwani ugaidi wote ni mbaya tu. Kwa upande wake Rais Park Geun-hye wa Korea Kusini ameitaja Iran kuwa na nafasi pana ya nguvu kazi, uwezo mkubwa wa kimapato, nafasi yake muhimu na ya kipekee ya kijografia na kuongeza kuwa, nchi yake inataraji katika mustakbali kuona mahusiano ya nchi mbili hizi yakistawi zaidi katika nyanja tofauti hususan katika sekta ya kiuchumi.