Meli kubwa zaidi ya kivita iliyoundwa Iran yazinduliwa rasmi
(last modified Wed, 13 Jan 2021 08:08:45 GMT )
Jan 13, 2021 08:08 UTC
  • Meli kubwa zaidi ya kivita iliyoundwa Iran yazinduliwa rasmi

Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo limepokea meli yake kubwa zaidi ya kivita ambayo imeundwa nchini Iran. Meli hiyo kubwa ya kivita ambayo imeundwa kikamlifu na wataalamu wa Iran ina uwezo wa kusheheni helikopta kadhaa kwa ajili ya oparehseni muhimu za baharini.

Meli hiyo imepewa jina la Makran, ambalo ni eneo la ukanda wa pwani ya kusini mwa Iran na imekabidhiwa Jeshi la Majini katika hafla ambayo imehuhduriwa na Mwenyekiti wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Meja Jenerali Muhammad Baqeri na Kamanda wa Jeshi la Iran Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi.

Kwa mujibu wa taarifa meli hiyo itakuwa na majukumu ya kutekeleza oparehseni katika maeneo ya mbali kama vile kaskazini mwa Bahari ya Hindi, Lango Bahari la Bab al-Mandab na Bahari ya Sham.

Meli hiyo kubwa zaidi ya kivita ya Iran mbali na kusheheni helikopta kadhaa pia itasheheni ndege za kivita zisizo na rubani na hali kadhalika mizinga.

Meli mpya ya kivita ya Iran yenye uwezo wa kusheheni helikopta 

Aidha imedokezwa kuwa meli hiyo mpya ya kivita ya Iran inaweza kutumika wakati wa dhoruba kali baharini na mbali na masuala ya kivita inaweza kutumika katika shughuli za uokoaji na shughuli zingine za kilojistiki za kuzisaidia meli zinginezo.

Manowari hii mpya ya Iran ina urefu wa mita 228, urefu wa juu wa mita 21.5 na upana wa mita 42.5 na hivyo kuifanya kuwa meli kubwa zaidi ya kivita ya Iran huku ikiwa na uwezo wa kuenda kasi ya noti 15. 

Leo pia Jeshi la Majini la Iran limeanza mazoezi makubwa ambayo yamepewa jina la Eqtedar-e-Daryayi yaani nguvu za baharini.

 

 

Tags