Iran yafanyia majaribio kombora la balistiki
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i6748-iran_yafanyia_majaribio_kombora_la_balistiki
Iran hivi karibuni ilifanyia majaribio kombora la balistiki lenye uwezo wa kuruka masafa ya kilomita 2,000 na kulenga shabaha kwa ustadi mkubwa.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 09, 2016 15:19 UTC
  • Iran yafanyia majaribio kombora la balistiki

Iran hivi karibuni ilifanyia majaribio kombora la balistiki lenye uwezo wa kuruka masafa ya kilomita 2,000 na kulenga shabaha kwa ustadi mkubwa.

Hayo yamedokezwa na  Naibu Mkuu wa Majeshi ya Iran Brigedia Jenerali Ali Abdollahi leo Jumatatu ambapo amebaini kuwa: " Wiki mbili zilizopita, tulifanyia jaribio kombora lenye uwezo wa kuruka kilomita 2,000 na lenye mwanya wa kasoro, (margin of error) ya mita nane."

Mara kwa mara majeshi ya Iran hufanyia majaribio makombora ya balistiki ili kuonyesha uwezo wa kujihami wa nchi hii.

Shirika la Habari la Reuters limeakisi habari hiyo na kusema katika kipindi cha mwaka moja uliopita, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inajitahidi kuimarisha uwezo na ustadi wa makobora yake.

Nchi za Magharibi hasa Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimekuwa zikikosoa majaribio ya makombora ya balisitiki Iran na kudai kuwa eti hmajaribio hayo yanakiuka azimio nambara 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baada ya mapatano ya nyuklia ya Iran yaliyofikiwa baina ya Iran na madola sita makubwa duniani.

Iran inasisitiza kuwa, makombora yake hayajaundwa kubebea vichwa vya nyuklia.