Jun 23, 2021 02:29 UTC
  • Chanjo ya Corona inayoundwa na IRGC ya Iran kuzinduliwa karibuni

Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 iliyozalishwa na Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) itazinduliwa ndani ya siku chache zijazo.

Meja Jenerali Mohammad Baqeri, Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema hayo jana na kuongeza kuwa, taasisi zote za vikosi vya ulinzi vya Iran ziko mbioni kupambana na virusi vya Corona.

Amebainisha kuwa, "Chanjo ya Wizara ya Ulinzi ipo katika marhala ya pili ya majaribio ya kliniki, na ile inayozalishwa na Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) itazinduliwa katika kipindi cha siku chache zijazo."

Chanjo ya Iran-Cuba imeripotiwa kuwa na uwezo wa kukabiliana na spishi zote za Corona

Iran iko katika mstari ya mbele kuunda chanjo za COVID-19 ambapo mbali na chanjo ya COV Iran Barakat, chanjo zingine ambazo zimepiga hatua nzuri katika majaribio ni pamoja na Razi Cov Pars, Fakhra na chanjo ya pamoja ya Taasisi ya Chanjo ya Finlay ya Cuba na Taasisi ya Chanjo ya Pasteur ya Iran.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Shirika la Dawa na Chakula la Iran, Dakta Kianoush Jahanpour, Jamhuri ya Kiislamu imejiunga na kundi la nchi chache duniani zinazozalisha chanjo ya ugonjwa wa COVID-19.

Tags