Amir-Abdollahian: Umoja wa Mataifa una jukumu la kutetea haki za Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i74490-amir_abdollahian_umoja_wa_mataifa_una_jukumu_la_kutetea_haki_za_wapalestina
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani jinai za utawala haramu wa Israel na kueleza kwamba, Umoja wa Mataifa una jukumu la kutetea haki za Wapalestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 10, 2021 03:41 UTC
  • Amir-Abdollahian: Umoja wa Mataifa una jukumu la kutetea haki za Wapalestina

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani jinai za utawala haramu wa Israel na kueleza kwamba, Umoja wa Mataifa una jukumu la kutetea haki za Wapalestina.

Hussein Amir-Abdollahian amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambapo ameashiria hatua za Israel na kueleza kwamba, utawala huo ghasibu unaendelea kutenda wazi na bayana jinai zake katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu .

Abdollahian ameeleza kuwa, Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa zina jukumu la kutetea malengo ya Palestina pamoja na haki za wanawake na watoto wasio na ulinzi wa Palestina.

Kuhusiana na mazungumzo ya Vienna Austria ya faili la makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, Amir-Abdollahian amesema, Marekani imekosea mahesabu kutokana na kuendeleza vikwazo vyake haramu dhidi ya Iran na inajidanganya kwa kudhani kwamba, inaweza kulitumia hilo kama wenzo wa mazungumzo na kufikioa malengo.

 

Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kusisitiza utayari wa taifa hili wa kushirikiana na Umoja wa Mataifa ameonyesha wasiwasi wake wa harakati za kigaidi nchini Afghanistan na eneo la Asia Magharibi kwa ujumla kutokana na baadhi ya madola yenye nguvu kutumia ugaidi kama silaha ya kufikia malengo yao.

Kwa upande wake Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa sambamba na kumpongeza Amir-Abdollahian kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, umoja huo unaunga mkono kwa dhati juhudi za Iran za kuwapokea wakimbizi.