Rais wa Iran aipongeza Afrika Kusini kwa kuadhimisha Siku ya Taifa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i83002-rais_wa_iran_aipongeza_afrika_kusini_kwa_kuadhimisha_siku_ya_taifa
Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia ujumbe wa pongezi mwenzake wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa kwa mnasaba wa taifa hilo la Kiafrika kuadhimisha Siku ya Taifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 27, 2022 22:20 UTC
  • Rais wa Iran aipongeza Afrika Kusini kwa kuadhimisha Siku ya Taifa

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia ujumbe wa pongezi mwenzake wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa kwa mnasaba wa taifa hilo la Kiafrika kuadhimisha Siku ya Taifa.

Jana Jumatano, Afrika Kusini iliadhimisha Siku ya Taifa, ambayo inafahamika pia kama Siku ya Uhuru nchini humo. Tarehe kama ya jana (Aprili 27) mwaka 1994, Afrika Kusini ilifanya uchaguzi wa kwanza baada ya kumalizika utawala wa kibaguzi wa apartheid.

Katika ujumbe huo kwa Rais Ramaphosa, Sayyid Ebrahim Raisi amesema: Natumai kwa uongozi wa Mheshimiwa Rais, serikali na taifa la Afrika Kusini litapiga hatua mbele kuelekea katika njia ya ustawi wa kijamii na kiuchumi, na wakati huohuo, tushuhudie kupanuka na kuimarika kwa uhusiano na ushirikiano wa pande mbili wa nchi mbili hizi. 

Kadhalika Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kuhusu mualiko wa kufanya ziara rasmi ya kuitembelea Afrika Kusini na kubainisha kuwa, anatumai safari hiyo itafungua njia za kustawi zaidi uhusiano wa Tehran na Pretoria.

Rais wa zamani wa Iran Hassan Rouhani (kulia) alipokutana na Ramaphosa

Hivi karibuni, Naledi Pandor, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini katika mazungumzo yake na mwenzake wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian, aliipongeza Jamhuri ya Kiislamu kwa kuiunga mkono nchi hiyo ya Kiafrika katika taasisi na mashirika ya kimataifa.

Hali kadhalika Bi Pandor mbali na kumualika Rais Ebrahim Raisi wa Iran kuitembelea Afrika Kusini alieleza kuwa, anatumai safari hiyo itaandaa mazingira ya kuimarika zaidi uhusiano wa pande mbili wa Tehran na Pretoria.