Kiongozi Muadhamu awataka wananchi kudumisha "moyo wa kimapinduzi"
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i8380-kiongozi_muadhamu_awataka_wananchi_kudumisha_moyo_wa_kimapinduzi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametoa wito kwa wananchi kulinda na kudumisha "moyo wa kimapinduzi" uliowatimua maadui nje ya nchi miaka 38 iliyopita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 03, 2016 03:43 UTC
  • Kiongozi Muadhamu awataka wananchi kudumisha

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametoa wito kwa wananchi kulinda na kudumisha "moyo wa kimapinduzi" uliowatimua maadui nje ya nchi miaka 38 iliyopita.

Ayatullah Khamenei ameyasema hayo mapema leo mbele ya hadhara ya waombolezaji zaidi ya milioni moja walioshiriki kwenye hauli ya mwaka wa 27 tangu alipoaga dunia mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini (ra) iliyofanyika kwenye haram ya shakhsia huyo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina maadui wengi wadogo na wakubwa, lakini wakubwa zaidi kati yao ni Marekani na Uingereza.

Ayatullah Khamenei ameashiria historia ya uadui wa Marekani ikiwemo kumuunga mkono Saddam katika vita dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, utunguaji ndege ya abiria ya Iran, kuvishambulia vituo vya mafuta vya Iran na mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) dhidi ya serikali halali nchini.

Ametadharisha kwa kusema:"Mtu yeyote au watu waliopo hivi sasa wanaofanya kazi kwa ajili ya Uislamu, wataharibikiwa vibaya endapo wataiamini Marekani".

Katika hotuba yake hiyo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza pia kwamba "Uchumi wa Muqawama" ndio njia pekee itakayoliwezesha taifa la Iran kuijtegemea kiuchumi na kuwataka viongozi nchini kuzingatia zaidi fursa na uwezo wa ndani ya nchi.../