Nov 24, 2022 07:35 UTC
  • Iran ni ya 10 duniani kwa kuzalisha magari madogo; yazipiku Uingereza na Ufaransa

Shirikisho la watengeza magari barani Ulaya limeitangaza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa taifa la kumi duniani kwa kuzalisha na kutengeneza magari madogo.

Shirikisho la watengeza magari barani Ulaya limeitangaza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa taifa la kumi duniani kwa kuzalisha na kutengeneza magari madogo.

Taarifa ya shirikisho hilo imeeleza kuwa, katika kipindi cha mwezi Januari mpaka Septemba mwaka huu, Iran ilizalisha magari mengi madogo na kuyapiku mataifa makubwa kama Ufaransa, Uingereza na Italia.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya sekta ya viwanda, katika kipindi cha kati ya Januari na Septemba mwaka huu jumla ya magari  49,817,000 yalitengenezwa na kuzalishwa duniani ambapo hisa ya Iran ilikuwa asilimia 1.9 na kuifanya ishike nafasi ya kumi duniani kwa kutengeneza magari madogo.

Katika mwaka uliopita na katika kiipindi cha Januari hadi Septemba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilishika nafasi ya 13 duniani kwa kuzalisha magari madogo. Hili ni ongezeko la asilimia 31.2 ikilinganishwa na mwaka jana.

 

Chama cha watengezaji magari barani Ulaya kimesema kuwa, mwaka huu hadi kufikia mwezi Septemba, Iran imeyapiku mataifa mengi katika kuzalisha magari madogo duniani kama Russia, Jamhuri ya Czech na Slovakia.

Aidha mataifa makubwa ya Ulaya kama Ufaransa, Uingereza na Italia yameachwa nyuma na Iran katika miezi tisa ya awali ya mwaka huu katika uga wa utengenezaji magari madogo.

Katika kipindi hiki Iran imeweza kutengeneza magari madogo ya kutembelea 949,726 huku Ufaransa ikitengeneza magari 693,000.

Jamhuri ya Kiislamu imeendelea kupiga hatua za ustawi na maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo ya utengezaji magari na kuongeza kiwango cha uzalishaji licha ya kuandamwa na vikkwazo vya kiuchumi na mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa ya Marekani na washirika wake.

Tags