Raisi: Damu toharifu za 'mashahidi wa usalama' zinawatia kiwewe maadui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i91504-raisi_damu_toharifu_za_'mashahidi_wa_usalama'_zinawatia_kiwewe_maadui
Rais wa Iran amesema damu toharifu za maafisa usalama wa Jamhuri ya Kiislamu waliouawa shahidi zimewakasirisha na kuwatia kiwewe maadui wa taifa hili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 09, 2022 22:53 UTC
  • Raisi: Damu toharifu za 'mashahidi wa usalama' zinawatia kiwewe maadui

Rais wa Iran amesema damu toharifu za maafisa usalama wa Jamhuri ya Kiislamu waliouawa shahidi zimewakasirisha na kuwatia kiwewe maadui wa taifa hili.

Rais Ebrahim Raisi alisema hayo jana Ijumaa katika kikao kilichofanyika kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kufa shahidi Bibi Fatimatu Zahra (AS), binti wa Mtume Muhammad (SAW), ambapo amezienzi familia za askari polisi na maafisa wengine wa usalama waliouawa shahidi katika machafuko ya hivi karibuni hapa nchini. 

Ameashiria kushindwa maadui katika vita vya miaka minane vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran na kueleza kuwa, maadui wanajaribu kuibua vita mseto na njama mpya ili kuchochea ghasia na mifarakano miongoni mwa wananchi wa Iran, lakini njama hizo zimegonga mwamba kutokana na kuwa macho taifa la Iran.

Rais wa Iran amesema maadui wa taifa hili kwa upande mmoja wanadai wanapigania 'haki ya kuishi'  na kwa upande mwingine wanaunga mkono magaidi wanaowaua maafisa usalama, wazazi na mtoto wa miaka 10.

Sayyid Ebrahim Raisi alikuwa anarejelea mauaji ya mtoto wa miaka 10, wazazi wake na watu wengine kadhaa katika shambulio la hivi karibuni la kigaidi kwenye Haram Takatifu ya Shah Cheragh mjini Shiraz, katika mkoa wa kusini wa Fars.

Rais Raisi akiongea na watoto wa maafisa usalama wa Iran waliouawa shahidi karibuni

Raisi amegusia ubeberu wa vyombo vya habari vya Magharibi na kusema kuwa, madai ya uhuru bandia ya Wamagharibi yameshindwa kupenya katika masikio na nyoyo za Wairani. Amesema kazi kubwa ya mashirika hayo ya habari ni kupotosha ukweli kwa kupindisha habari na kusema urongo.

Amesema Marekani ilivamia na kukalia kwa mabavu Afghanistan kwa miongo kadhaa kwa madai ya kutaka kuleta demokrasia katika nchi hiyo, lakini matokeo yake yakawa ni kuuawa watoto 35,000 na kuharibiwa nyumba nyingi za Waafghani.