Jan 01, 2023 12:24 UTC
  • Nusu ya watu bilioni moja wa nchi za eneo ni wateja wa mazao ya kilimo ya Iran

Mkuu wa Kamisheni ya Kilimo, Maji, Maliasili na Mazingira katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa zaidi ya watu milioni 500 katika nchi za kanda hii na jirani zake wanataka kunufaika na bidhaa za kilimo za Iran.

Muhammad Javad Asgari Mkuu wa Kamisheni ya Kilimo, Maji, Maliasili na Mazingira katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema leo katika Mkutano wa Sekta ya Mifugo katika mkoa wa Farsi kusini mwa Iran kwamba mkoa huo umechaguliwa kama kituo cha kuuza nje mazao ya kilimo na kwamba hakupasi kuwepo marufuku yoyote katika uuzaji nje mazao ya kilimo bali mkakati uliopo ni kutatua matatizo yanayokwamisha suala hilo. 

Mwakilishi huyo wa wananchi katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge)  ameongeza kuwa kwa kujibu wa mpango wa majlisi, Wizara ya Jihadi ya Kilimo inawajibika kusaidia usafirishaji wa mazao ya kilimo nje ya nchi na kuondoa baadhi ya vikwazo na vizuizi vilivyopo.

Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) limetoa takwimu mpya zinazoonyesha kuwa Iran ni miongoni mwa nchi wazalishaji wakubwa wa mazao ya kilimo duniani. Shirika la FAO aidha limetangaza kuwa, licha ya ukame uliopo, Iran ilishika nafasi ya tarakimu moja duniani mwaka juzi wa 2021 katika kuzalisha mazao 20 ya kilimo. Ripoti ya FAO imeongeza kuwa, Iran mwaka juzi ilishika nafasi nzuri duniani kwa upande wa kuzalisha aina mbalimbali za mazao ya kilimo.    

Tags