Rais wa Iran: Syria imeibuka na ushindi licha ya vitisho na vikwazo
(last modified Wed, 03 May 2023 11:40:57 GMT )
May 03, 2023 11:40 UTC
  • Rais wa Iran:  Syria imeibuka na ushindi licha ya vitisho na vikwazo

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, serikali ya Syria pamoja na wananchi wa nchi hiyo wamepitia masaibu na matatizo mengi na hii leo taifa hilo limeweza kuibuka ushindi.

Rais Ebrahim Raisi amesema hhayo leo mjini Damascus katika mazungumzo yake na Rais Bashar al-Assa wa nchi hiyo na kubainisha kwamba, hii leo tunaweza kusema kwamba, Syria imevuka matatizo yote ya vikwazo na vitishho na imeibuka na ushindi.

Rais wa Iran ambaye leo aliwasili nchini Syria na kupokewa na mwenyeji wake katika ziara rasmi ya siku mbili amesema pia kuwa, uhusiano wa Damascus na Tehran  ni wa kidugu na umeendelea kuwa hivyo licha ya kimbunga cha kisiasa na kiusalama kilicholikumba eneo la Asia Magharibi.

Aidha amesema, kama ambavyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikuwa pamoja na Syria katika vita dhidi ya ugaidi itakuwa pamoja na serikali na wananchhi wa nchi hiyo pia katika kuikarabati na kuijenga tena nchi hiyo.

Rais wa Iran akikaribishwa rasmi na mwenyeji wake Bashar al-Assad

 

Kwa upande wake Rais Bashar al-Assad wa Syria amepongeza na kuthamini misimamo na himaya ya Jamhuri ya Kiislamu kwa serikali na wananchi wa Syria katika masiku magumu na ya mgogoro na kubainisha kwamba, serikali na wananchi wa nchi hiyo katu hawawezi kusahauu huba, mapenzi na misaada ya Tehran kwao.

Marais hao wamejadili pia kwa kina matukio ya hivi karibuni katika eneo la Asia Magharibi na njia za kuboresha zaidi uhusiano na ushirikiano baina yao katika nyanja mbalimbali.

Tags