May 08, 2023 06:28 UTC
  • Kana'ani Chafi: Kuuawa Wapalestina limekuwa jambo la kawaida la kila siku kwa Wazayuni

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, matokeo ya kimya cha wanaodai kuwa watetezi wa haki za binadamu kuhusiana na mauaji dhidi ya Wapalestina kumefanya kuuawa Wapalestina hao kuwa jambo la kawaida na la kila siku la Wazayuni.

Nasser Kana'ani Chafi amesema hayo katika ujumbe wake aliuandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter na kueleza kwamba, asasi za kimataifa hususan Umoja wa Mataifa una jukumu la kisheria la kuwahami na kuwatetea Wapalestina mkabala na utawala ghasibu wa Israel.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali vitendo vya kila leo vya hujuma na mauaji ya askari wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.

Wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel kila siku wamekuwa wakiwashambulia, kuwatia mbaroni, kuwajeruhi sambamnba na kuwaua shahidi wananchi wa Palestina wakitumia visingizo mbalimbali.

 

Katika miezi ya hivi karibuni hujuma na mashambulio ya utawala vamizi wa Israel dhidi ya Wapalestina yamechukua wigo mpana zaidi huku mataifa huru yakizioonyeshea kidole cha lawama asasi za kimataifa kutokana na kimya chao na kutochukua hatua yoyote ya kukabiliana na jinai za utawala huo ghasibu.

Wakati huo huo, vitendo vya hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa vimekithiri zaidi baada ya kuingia madarakani serikali yenye misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu ambayo imekuwa ikionyesha chuki za wazi wazi dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.

Tags