Hizbullah: Utawala wa Kizayuni lazima ufutwe katika eneo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i101394-hizbullah_utawala_wa_kizayuni_lazima_ufutwe_katika_eneo
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria hatari ya utawala wa Kizayuni kwa jamii ya mwanadamu na kusisitiza kuwa, utawala huo haramu unapaswa kufutwa katika uso wa eneo la Asia Magharibi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 23, 2023 06:50 UTC
  • Hizbullah: Utawala wa Kizayuni lazima ufutwe katika eneo

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria hatari ya utawala wa Kizayuni kwa jamii ya mwanadamu na kusisitiza kuwa, utawala huo haramu unapaswa kufutwa katika uso wa eneo la Asia Magharibi.

Sheikh Naim Qassim amenukuliwa akisema hayo leo Jumatano na shirika la habari la Al-Manar na kuongeza kuwa, "Utawala wa Israel unapasa kufutwa kikamilifu katika eneo, kwa kuwa utawala huo si tu ni hatarishi kwa dunia, lakini pia kwa ubinadamu na mustakabali." 

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo pia na kuandika kuwa, Sheikh Qassim amesema Harakati ya Muqawama ya Hizbullah imebadilisha mlingano wa nguvu katika eneo hili la kistratejia.

Ameeleza bayana kuwa, muqawama ni moja ya nguzo kuu za  amani na nguvu ya Lebanon na vile vile imechangia katika uthabiti wa eneo la Asia Magharibi mkabala wa njama za Wazayuni.

Mwanachuoni huyo wa Kiislamu nchini Lebanon amesema kuungana na kushikamana Waislamu pasina kujali tofauti zao za kimitazamo na kiitikadi kumesambaratisha njama za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel za kuyagawanya vipande vipande mataifa ya Kiislamu.

Kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon imekuja baada ya gazeti la Kizayuni la Hayom kukiri katika makala yake ya karibuni kuwa, jeshi la utawala haramu wa Israel halina uwezo wa kuikabili kijeshi Hizbullah, kutokana na changamoto mbalimbali zinazougubika utawala huo pandikizi kwa sasa.

Mapema mwezi huu, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon aliionya vikali Israel na kusisitiza kuwa, utawala huo wa Kizayuni utarejeshwa nyuma mamilioni ya miaka hadi enzi za mawe, iwapo utaingia katika vita vipya na Lebanon.