Jihad Islami: Kukamatwa na mauaji ya kigaidi havizuii mapambano ya ukombozi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i101456-jihad_islami_kukamatwa_na_mauaji_ya_kigaidi_havizuii_mapambano_ya_ukombozi
Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesisitiza kuwa kukamatwa, ukandamizaji na mauaji ya kigaidi haviwezi kuzima moto wa mapambano ya ukombozi wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 25, 2023 04:30 UTC
  • Jihad Islami: Kukamatwa na mauaji ya kigaidi havizuii mapambano ya ukombozi

Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesisitiza kuwa kukamatwa, ukandamizaji na mauaji ya kigaidi haviwezi kuzima moto wa mapambano ya ukombozi wa Palestina.

Walid Al-Qutatti amesema katika hotuba yake jana Alkhamisi kwamba: Kukamatwa, kukandamizwa, mauaji ya kigaidi, kushambuliwa Msikiti wa Al-Aqswa na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi ya Palestina ni jaribio lililofeli la wavamizi wa Kizayuni la kutaka kuzima moto wa Muqawama na kusitisha mapambano yanayoongeza ya taifa la Palestina.

Huku akieleza kuwa adui Mzayuni amepoteza mlingano wa kiakili, Al-Qatati ameongeza kuwa: Harakati ya Jihad Islami itakabiliana ipasavyo na vitisho vya mara kwa mara vya utawala wa Kizayuni na kujibu vitisho hivyo.

Wapiganaji wa Jihad Islami

Al-Qatatti amewatahadharisha wanachama wa harakati za Muqawama kuhusu kuendelezwa mauaji ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ndani na nje ya Palestina, na kusema: Utawala wa Kizayuni umejaribu mbinu zote za jinai tokea kuasisiwa kwake na haujaweza kulizuia taifa la Palestina kuendeza mapambano ya ukombozi; na kushindwa huku ni ishara ya mgogoro mkubwa wa utawala huo kisiasa na kiusalama.

Mwanachama huyo wa ngazi ya juu wa harakati ya Jihad Islami amesisitiza kuwa: Taifa la Palestina halitaacha mapambano hadi litakapokomboa kikamilifu ardhi yake kutoka kwenye makucha ya wavamizi, na kwamba harakati zote za makundi ya muqawama ndio tafsiri ya irada na azma ya taifa hilo.

Awali, Avigdor Lieberman, mkuu wa chama cha "Yisrael Beiteinu", alizungumzia operesheni ya hivi karibuni ya wanamapambano wa Palestina katika mji wa "Hawarah" ulioko kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, ambapo Wazayuni 2 waliuawa, na akatoa wito kwa utawala wa Kizayuni kurejea kwenye siasa za kuwauwa viongozi wa Hamas.