Askari wa Israel wawashambulia waandamanaji wa Kipalestina, 30 wajeruhiwa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i102562-askari_wa_israel_wawashambulia_waandamanaji_wa_kipalestina_30_wajeruhiwa
Wanajeshi makatili wa utawala haramu wa Israel wamewashambulia waandamanaji wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza na kujeruhi 30 miongoni mwao.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Sep 23, 2023 04:11 UTC
  • Askari wa Israel wawashambulia waandamanaji wa Kipalestina, 30 wajeruhiwa

Wanajeshi makatili wa utawala haramu wa Israel wamewashambulia waandamanaji wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza na kujeruhi 30 miongoni mwao.

Wapalestina hao walikusanyika jana Ijumaa katika mpaka wa Gaza na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, kushiriki maandamano ya kulaani jinai za Wazayuni dhidi yao. 

Jeshi la utawala wa Kizayuni limetangaza kuwa limefanya mashambulizi ya anga dhidi ya Ukanda wa Gaza. Limedai kuwa, shambulizi moja la ndege isiyo na rubani (droni) limelenga kambi za kijeshi za Harakati ya Muqawama ya Hamas inayotawala Gaza.

Wizara ya Afya ya Palestina imesema Wapalestina 30 wamejeruhiwa kwenye mashambulizi hayo ya kikatili ya wanajeshi wa Israel, ambayo yamekuja siku chache baada ya muandamanaji mmoja wa Kipalestina kuuawa shahidi kwa kupigwa risasi na askari wa Kizayuni.

Aidha jana Ijumaa, Abdullah Emad Abu al-Hasan, kijana Mpalestina aliyekuwa na umri wa miaka 18, aliga dunia kutoka na majeraha ya risasi alizopigwa na wanajeshi wa Israel, walipokuwa wanakabiliana na waandamanaji wa Kipalestina katika kitongoji cha Kafr Dan, yapata kilomita 8 kaskazini magharibi mji wa Jenin, katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu.

Haya yanajiri siku chache baada ya wanajeshi hao vamizi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuwaua shahidi Wapalestina wanne katika mashambulizi mawili tofauti katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza.

Wimbi hilo la ukatili wa wanajeshi wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi limejiri wakati huu ambapo Wapalestina wameendelea kuandamana katika mpaka wa Gaza kulaani jinai za Wazayuni, kuendelea kuzuiliwa Wapalestina kinyume cha sheria, na kuuvunjia heshima Msikiti Mtukufu wa al-Aqsa.