Idadi ya mashahidi wa Palestina Gaza yapindukia 3500
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103682-idadi_ya_mashahidi_wa_palestina_gaza_yapindukia_3500
Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, zaidi ya Wapalestina 3,500 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 13,000 kujeruhiwa kutokana na hujuma na mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 19, 2023 11:17 UTC
  • Idadi ya mashahidi wa Palestina Gaza yapindukia 3500

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, zaidi ya Wapalestina 3,500 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 13,000 kujeruhiwa kutokana na hujuma na mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza leo kuwa,  Wapalestina wasiopungua 3,785 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 13,000 kujeruhiwa katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa uvamizi wa utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, ambao umekuwa ukiendelea kwa siku 13.

Wizara ya Afya wa Palestina imeongeza kuwa, utawala wa Kizayuni hadi sasa umetahadharisha kuhusu kuhamishwa hospitali 24 za Gaza ikiwemo Hospitali ya Al-Shafa.

Wakati hhyuo huo, juzi usiku utawala wa Kizayuni wa Israel ulifanya jinai isiyo na kifani kwa kushambulia Hospitali ya al-Ma'madani katika Ukanda wa Gaza kwa bomu lenye uzito wa tani moja na kuua shahidi raia karibu elfu moja na mia moja.

Jinai hiyo iliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel imetajwa kuwa ndio holocaust halisi.

 

Utumiaji wa bomu hilo la Marekani lenye uzito wa tani moja umeifanya idadi ya wahanga wa Hospitali ya Ma’madani kuwa kubwa mara nne zaidi ya uhalifu na jinai ya Deir Yassin, mwaka 1948.

Utawala wa Kizayuni wa Israel uliishambulia kwa bomu hospitali hiyo wakati ukijua kuwa, kulikuwa na wagonjwa na majeruhi wengi ndani ya hospitali hiyo. Utawala wa Kizayuni ulilenga kwa makusudi hospitali hiyo ili kufidia kushindwa na kipigo cha aina yake katika operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa; hata hiyo jinai ya Al-Ma’madani imedhihirisha tena sura ya kinyama na ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni mbele ya macho ya walimwengu.

Wizara hiyo pia ilitangaza kwamba idadi ya wafia dini na waliojeruhiwa chini ya vifusi ni kubwa zaidi ya ile inayochapishwa.