Misaada ya kwanza ya kibinadamu yaingia Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103760-misaada_ya_kwanza_ya_kibinadamu_yaingia_ukanda_wa_gaza
Awamu ya kwanza ya misaada ya kibinadamu imeingia katikak ukanda wa Gaza huko Palestina na kuleta ahueni ya namna fulani kwa wananchi hao wanaokabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 21, 2023 09:57 UTC
  • Misaada ya kwanza ya kibinadamu yaingia Ukanda wa Gaza

Awamu ya kwanza ya misaada ya kibinadamu imeingia katikak ukanda wa Gaza huko Palestina na kuleta ahueni ya namna fulani kwa wananchi hao wanaokabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu.

Malori ya kwanza yaliyobeba bidhaa za misaada leo yameingia Ukanda wa Gaza kupitia mpaka wa Rafah ulioko kati ya Misri na ukanda huo.

Ripoti zinasema kuuwa, malori 20 yanayobeba bidhaa za matibabu yamewasili huko Gaza. Huo ni msaada wa kwanza wa kibinadamu kupelekwa katika ene

 

o hilo tangu kuzuka kwa vita kati ya Israel na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya palestina HAMAS wiki mbili zilizopita.

Kulikuwa na miito ya Gaza kupatiwa misaada ya kibinadamu haraka baada ya Israel kuzuia uingizwaji wa mahitaji muhimu yakiwemo maji, chakula, dawa na nishati ya mafuta.

Kivuko cha Rafah kimefunguliwa huku picha za moja kwa moja zikionyesha malori yakiingia kwenye mpaka kutoka Misri kuelekea Gaza.

Haijulikani ni kwa muda gani kivuko kitabaki wazi. Utawala hharamu wa Israel hadi sasa umekubali kuruhusu malori 20 kuingia Gaza.

Malori hayo yamebeba chakula, maji na dawa lakini hayana mafuta na yanaingia Gaza kupitia kivuko cha kusini kutoka Misri.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limeyatuhumu madola ya Magharibi kwa kile ilichosema kuwa unafiki na undumakuwili kwa kushindwa kukemea jinai zinazofanywa na utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Hii leo wale wanaodai kutetea haki za binadamu na ambao wanatekeleza malengo yao ya kisiasa kwa kutumia mashinikizo wameifumbia macho kabisa Gaza na dhulma inayofanywa dhidi ya wananchi wa Palestina.