Hizbullah: Ukanda wa Gaza utakuwa kaburi la utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103782-hizbullah_ukanda_wa_gaza_utakuwa_kaburi_la_utawala_wa_kizayuni
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya nchini Lebanon amesema jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza hazitapita hivi hivi bila kupatiwa jibu na kusisitiza kuwa, eneo hilo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu litageuka na kugeuka na kuwa kaburi la kuuzika utawala huo bandia.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Oct 21, 2023 23:52 UTC
  • Hizbullah: Ukanda wa Gaza utakuwa kaburi la utawala wa Kizayuni

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya nchini Lebanon amesema jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza hazitapita hivi hivi bila kupatiwa jibu na kusisitiza kuwa, eneo hilo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu litageuka na kugeuka na kuwa kaburi la kuuzika utawala huo bandia.

Sheikh Naim Qassim amenukuliwa akisema hayo na shirika la habari la Iran Press na kuongeza kuwa: Maadui zetu ni waoga, na wanatiwa kiwewe na nguvu za muqawama; kwa msingi huo wapo katika mkondo wa kuporomoka.

Sheikh Qassem ameeleza bayana kuwa, "Opereseheni ya Kimbunga cha al-Aqsa imepata mfanikio ya aina yake na ambayo yatabaki hai mpaka utawala wa Kizayuni utokomezwe kikamilifu."

Kadhalika kiongozi huyo wa Kiislamu wa Lebanon amebainisha kuwa, Wamagharibi wanaunga mkono jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni, na hilo linawafanya kuwa washirika wa Wazayuni katika jinai zake dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Amesema: Wamagharibi wanazuia uamuzi wowote wa kulaani jinai za utawala ghasibu wa Israel, na kwa msingi huo, wanabeba dhima kamili ya jinai zinazofanywa na utawala huo pandikizi.

Jinai za Israel Ukanda wa Gaza

Kauli ya Sheikh Naim Qassim inakuja siku chache baada ya viongozi wa Marekani akiwemo Rais Joe Biden kuwatahadharisha watawala wa Israel kuhusu ugumu na hatari ya kuendesha vita viwili kwa wakati mmoja, huko kusini na Hamas na upande wa kaskazini na harakati yenye nguvu kubwa ya kijeshi ya Hizbullah.

Wiki iliyopita, Hizbullah ya Lebanon ilitangaza kuwa imetoa kipigo kikali katika mashambulio iliyofanya dhidi ya ngombe za jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika mashamba ya Shabaa ya ardhi ya Lebanon inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo.