HAMAS yakanusha madai ya Netanyahu kuhusu kufichwa mateka mahospitalini
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i104908-hamas_yakanusha_madai_ya_netanyahu_kuhusu_kufichwa_mateka_mahospitalini
Brigedi za al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimekanusha madai ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu aliyedai kuwa Wapalestina walikuwa wamewaficha mateka Wazayuni kwenye hospitali za Ghaza ili kuhalalisha jinai zake dhidi ya watoto wachanga na wagonjwa kwenye hospitali hizo. 
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 18, 2023 00:19 UTC
  • HAMAS yakanusha madai ya Netanyahu kuhusu kufichwa mateka mahospitalini

Brigedi za al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimekanusha madai ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu aliyedai kuwa Wapalestina walikuwa wamewaficha mateka Wazayuni kwenye hospitali za Ghaza ili kuhalalisha jinai zake dhidi ya watoto wachanga na wagonjwa kwenye hospitali hizo. 

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, Abu Ubaidah, Msemaji wa Brigedi za Izzuddin al Aqassam amesema kuwa, waziri mkuu wa Israel na msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni ni waongo wanapodai kuwa HAMAS imeficha mateka wa Kizayuni kwenye hospitali za Ghaza.

Amesema, kilichofanyika ni kwamba hali za kiafya za baadhi ya mateka Wazayuni zilikuwa mbaya sana, hivyo HAMAS ililazimika kuwapeleka kwenye kutibiwa hospitalini na baada ya kutibiwa iliwarejesha sehemu zao.

Amesema, mashambulio ya mara kwa mara ya Israel dhidi ya maeneo yaliyoko karibu na sehemu walipofichwa mateka, yamesababisha baadhi yao kujeruhiwa na kuuawa na kwamba katika siku za usoni HAMAS itasambaza ushahidi madhubuti kuhusu jambo hilo.

Bi Kizee wa Israel akiwashukuru HAMAS kwa muamala mzuri waliomfanyia

 

Waziri Mkuu wa Israel amelazimika kujitoa kimasomaso baada kukumbwa na mashinikizo makubwa kufuatia amri yake ya kuvamiwa Hospitali ya al Shifaa na wanajeshi makatili wa Israel. Awali Wazayuni walidai kuwa HAMAS imezigeuza hospitali za Ghaza kuwa kambi zake za kijeshi, na baada ya kukosa ushahidi wa kuhalalisha jinai na mashambulizi yake kwenye hospitali hizo, wamedai kuwa, HAMAS ilikuwa imeficha mateka wa Kizayuni kwenye hospitali hizo, na hivi sasa baada ya kuthibitika uongo wao, Benjamin Netanyahu anadai kuwa eti walikuwa na taarifa za uhakika kuwa mateka wamefichwa hospitalini. 

HAMAS wamekanusha uongo huo wa Wazayuni na kusisitiza kuwa, hakuna mateka yeyote waliyemficha hosptalini na kwamba jinai za Israel za kushambulia kikatili hospitali na maeneo ya umma, hazihalalishiki kivyovyote vile.