Muqtada Sadr atahadharisha juu ya kutumwa askari wa US, Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i11473-muqtada_sadr_atahadharisha_juu_ya_kutumwa_askari_wa_us_iraq
Kiongozi wa Kiislamu nchini Iraq ameitahadharisha Marekani dhidi ya kutuma askari wake zaidi nchini humo kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 18, 2016 03:14 UTC
  • Muqtada Sadr atahadharisha juu ya kutumwa askari wa US, Iraq

Kiongozi wa Kiislamu nchini Iraq ameitahadharisha Marekani dhidi ya kutuma askari wake zaidi nchini humo kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.

Muqtada al-Sadr, amewaasa wafuasi wake kukabiliana na askari vamizi wa Marekani watakaotia mguu nchini humo eti kwa lengo la kuzima harakati za kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh. Hivi karibuni, Ashton Carter, Waziri wa Ulinzi wa Marekani alisema Washington itatuma askari 560 zaidi wa nchi hiyo kujiunga na juhudi za kukomboa mji wa Mosul toka mikononi mwa Daesh.

Sayyid Sadr amekuwa akisisitiza kuwa, kundi la kigaidi la Daesh ni mwana wa Marekani na Israel katika Mashariki ya Kati na kwamba, kundi la kigaidi la Daesh lilianzishwa kwa ajili ya kulinda maslahi ya Marekani na Israel katika eneo hili. Muqtada al Sadr ameashiria kimya na hata misaada na uungaji mkono wa ndege za muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani kwa magaidi wa kundi hilo la kitakfiri huko Iraq na kusema kuna udharura wa kutokomezwa kabisa ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.