OIC yasema, Israel 'inabeba dhima kamili' ya mauaji ya Kiongozi wa HAMAS Ismail Haniya
(last modified 2024-08-08T06:32:40+00:00 )
Aug 08, 2024 06:32 UTC
  • OIC yasema, Israel 'inabeba dhima kamili' ya mauaji ya Kiongozi wa HAMAS Ismail Haniya

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeulaumu utawala wa Kizayuni wa Israel kwa shambulizi la kigaidi lililomuua Ismail Haniya, Mkuu wa Tawi la Kisiasa la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wiki iliyopita nchini Iran, ambayo Tehran imeapa kuyalipizia kisasi.

Mbali na kulaani mauaji hayo, taarifa iliyotolewa jana Jumatano baada ya kikao cha dharura cha jumuiya hiyo yenye wanachama 57 kilichofanyika nchini Saudi Arabia imesema "inaibebesha Israel, utawala unaokalia ardhi kwa mabavu, dhima kamili ya shambulio hilo ovu sana", ambalo imelitaja kuwa ni "ukiukaji mkubwa" wa mamlaka ya kujitawala ya Iran.
Kikao cha dharura cha OIC mjini Jeddah kimeitishwa kwa wito uliotolewa na Iran na Palestina.
Image Caption

 

Katika kikao hicho cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC, Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Hissein Brahim Taha, mbali na kulaani mauaji ya Ismail Haniya na ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uliofanywa na utawala wa Kizayuni katika amesema, jinai hiyo ovu iliyofanywa na utawala huo ni mwendelezo wa jinai za kivita na mauaji ya kimbari yanayofanywa kila leo na utawala huo ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza, Ukingo wa Magharibi na Baitul Muqaddas.
 
Katika taarifa ya mwisho wa kikao hicho OIC imetahadharisha pia kuhusu upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kusisitiza kuendeleza mshikamano wake imara na taifa la Palestina.
 
Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas na mmoja wa walinzi wake waliuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi iliyotokea mjini Tehran alfajiri ya kuamkia Jumatano, tarehe 31 Julai.../

 

Tags