Muendelezo wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za muqawama wa Kiislamu wa Iraq dhidi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel)
(last modified 2024-10-10T05:35:57+00:00 )
Oct 10, 2024 05:35 UTC

Muqawama wa Kiislamu wa Iraq kwa mara nyingine tena umelenga na kushambulia moja ya maeneo muhimu kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) kwa ndege isiyo na rubani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Muqawama wa Kiislamu wa Iraq umetangaza katika taarifa yake kwamba, Mujahidina wa kundi hilo kwa kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na Lebanon na vile vile katika kukabiliana na jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya raia wakiwemo watoto, wanawake na wazee, kwa kutumia ndege zisizo na rubani, Alhamisi hii asubuhi wamelenga shabaha muhimu kaskazini mwa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.

Hili ni shambulio la pili la muqawama wa Kiislamu wa Iraq katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu katika saa chache zilizopita, jambo ambalo limethibitishwa na wanamuqawama wa Kiislamu wa Iraq.

Jumatano usiku,  muqawama wa Kiislamu wa Iraq ulilenga shabaha nyingine muhimu huko Umm al-Rashrash (Eilat)  kusini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kwa ndege isiyo na rubani.

Mnamo tarehe 29 Septemba, wanamapambano wa muqawama wa Kiislamu wa Iraq vilr vilr walishambulia Umm al-Rasrash kwenye pwani ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa kutumia ndege kadhaa zisizo na rubani.
Ikumbukwe kuwa muqawama wa Kiislamu wa Iraq hapo awali ulionya kwamba, iwapo utawala wa Kizayuni utaendelea na mashambulizi yake ya kinyama na jinai katika Ukanda wa Gaza na Lebanon, utazidisha oparesheni zake dhidi ya vituo vya kijeshi vya utawala huo habithi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).

Tags