Daesh yafanya jinai kubwa katika mji wa Mosul, Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i1375-daesh_yafanya_jinai_kubwa_katika_mji_wa_mosul_iraq
Kundi la kigaidi la Daesh limewanyonga raia zaidi ya elfu moja katika eneo la Mosul huko Iraq.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 16, 2016 11:39 UTC
  • Daesh yafanya jinai kubwa katika mji wa Mosul, Iraq

Kundi la kigaidi la Daesh limewanyonga raia zaidi ya elfu moja katika eneo la Mosul huko Iraq.

katika hatua iliyotajwa kuwa haijawahi kufanywa na kundi hjilo kundi hilo la Daesh limezitaarifu familia za wafungwa zaidi ya elfu moja waliokuwa wakishikiliwa huko Mosul katika mkoa wa Nainawa kaskazini magharibi mwa Iraq kwamba limewanyonga wafungwa hao na kwamba wasisubiri tena kuachiwa huru wafungwa hao.

Magaidi wa Daesh baadaye waliizika miili ya wahanga hao katika makaburi ya umati huko kusini na magharibi mwa mji wa Mosul.

Mwezi Aprili mwaka jana, kundi la kigaidi la Daesh liliwanyonga wakazi karibu 2100 wa mji wa Mosul. Kundi hilo la kigaidi likiungwa mkono na baadhi ya nchi za Magharibi na za Kiarabu liliingia nchini Iraq yapata miaka miwili iliyopitana kuyakalia kwa mabavu baadhi ya maeneo ya nchi hiyo ukiwemo mji wa Mosul na kutenda jinai za kutisha.