Saudia ilishambulia kwa makusudi kikao cha maombolezo mjini Sanaa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i17230-saudia_ilishambulia_kwa_makusudi_kikao_cha_maombolezo_mjini_sanaa
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Saudi Arabia ilishambulia kwa makusudi kikao cha khitma na maombolezo mjini Sanaa ambapo mamia ya watu waliuawa na kujeruhiwa siku ya Jumamosi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 12, 2016 00:36 UTC
  • Saudia ilishambulia kwa makusudi kikao cha maombolezo mjini Sanaa

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Saudi Arabia ilishambulia kwa makusudi kikao cha khitma na maombolezo mjini Sanaa ambapo mamia ya watu waliuawa na kujeruhiwa siku ya Jumamosi.

Akizungumza mjini Beirut kwa njia ya televisheni katika mkesha wa maombolezo ya Ashura ya Imam Hussein AS, Sayyid Hassan Nasrallah aliashiria hujuma hiyo ya Jumamosi ya Saudia mjini Sanaa na kusema ndege vamizi za Saudia, mchana kweupe, zilivamia ukumbi mkubwa walimokuwa wamekusanyika waombolezaji na kudondosha mabomu ambapo idadi kubwa ya watu waliuawa shahidi.

Sayyid Nasrallah ameongeza kuwa Saudia imegonga mwamba katika malengo yake ya kuihujumu Yemen kwani watawala wa Riyadh walidhani kuwa, baada ya kuanza hujuma yao dhidi ya nchi hiyo Machi 2015, vita vingechukua wiki kadhaa kisha wapate ushindi lakini walifanya kosa kubwa la kistratijia kwani hawajapata ushindi na vita vinaendelea.

Hujuma ya Saudia kaskazni mwa Sanaa, Yemen

Sayyid Nasrallah amesema mwaka moja na nusu sasa tokea Saudia ianzishe hujuma za kinyama dhidi ya Yemen, watu madhulumu katika nchi hiyo wanazidi kuteseka huku jamii ya kimataifa ikinyamazia kimya ukatili wa Saudia. Kuhusu kadhia ya Syria, Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema Saudia inalenga kulinda maslahi ya utawala haramu wa Israel katika kuwaunga mkono magaidi ili wamuondoe madarakni Rais  Bashar al Assad.

Sayyid Nasrallah amesema iwapo taifa la Syria lingesalimu amri mbele ya magaidi, nchi hiyo ingeshuhudia umwagikaji mkubwa wa damu sasa na siku za usoni.