Marekani, Israel, Saudia zinachochea fitna Mashariki ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i2275-marekani_israel_saudia_zinachochea_fitna_mashariki_ya_kati
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na Saudi Arabia zinachochea fitna na mizozo ya kimadhehebu katika eneo nyeti la Mashariki ya Kati.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 02, 2016 02:50 UTC
  • Marekani, Israel, Saudia zinachochea fitna Mashariki ya Kati

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na Saudi Arabia zinachochea fitna na mizozo ya kimadhehebu katika eneo nyeti la Mashariki ya Kati.

Televisheni ya al Mayadeen ya nchini Lebanon imemnukuu Sayyid Hassan Nasrullah akisema hayo jana kwenye hotuba yake aliyoitoa kwa njia ya televisheni na kuongeza kuwa: Kuna taarifa zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kutokea mambo yasiyo sahihi katika baadhi ya maeneo ya Lebanon, lakini taarifa hizo zote ni za uongo, na hakuna matukio kama hayo yaliyotokea nchini Lebanon tarehe 7 Mei kama inavyodaiwa.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, Saudia inachochea fitna za kimadhehebu kati ya Waislamu, suala ambalo limekuwa likifanywa kwa muda mrefu na utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani.

Amesema, muqawama unalaani kitendo chochote cha kuvunjia heshima nembo za Kiislamu na kwamba suala hilo si kosa tu, bali ni dhambi.

Amesema kuna watu wanajaribu kuchochea fitna za kimadhehebu baina ya Waislamu kwa msaada wa kifedha wa Marekani, Saudia na Israel, na hiyo ni hatari kubwa sana kwa ulimwengu wa Kiislamu.