HRW yapinga uanachama wa Saudia katika Baraza la Haki za Wanawake la UN
(last modified Tue, 25 Apr 2017 03:43:41 GMT )
Apr 25, 2017 03:43 UTC
  • HRW yapinga uanachama wa Saudia katika Baraza la Haki za Wanawake la UN

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) amepinga vikali uanachama wa utawala wa Saudi Arabia katika Baraza la Haki za Wanawake la Umoja wa Mataifa.

Hillel Neuer amesema kuwa, ni jambo la kushangaza kuona Saudi  Arabia ambayo inafanya ubaguzi na ina sheria za kibaguzi dhidi ya wanawake, ikikubaliwa kama mwanachama wa Baraza la Haki za Wanawake, ambayo ni jumuiya kubwa zaidi ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu.

Hillel Neuer amehoji, ni kwa nini Umoja wa Mataifa umeikubaki Saudi Arabia inayoeneza dhulma na ukosefu wa usawa dhidi ya wanawake, kama mwanachama wa Baraza la Haki za Wanawake?

Hillel Neuer

Saudi Arabia ni miongoni mwa nchi zinazokandamiza na kukanyaga waziwazi haki za wanawake. Hata hivyo inashangaza kuwa, Umoja wa Mataifa umeipatia nchi hiyo uanachama katika Baraza lake la Haki za Wanawake. 

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Baraza la Haki za Wanawake la Umoja wa Mataifa, Saudia imeshika nafasi ya 4 kutoka mwisho kati ya nchi 144 kwenye orodha ya vigezo vya kimataifa vya hitilafu za kijinsia duniani katika mwaka uliopita wa 2016.   

Tags