Jul 08, 2017 07:55 UTC
  • Hizbullah: Marekani na EU zinazuia wakimbizi wa Syria kurejea nchini kwao

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani na Umoja wa Ulaya zimekuwa zikizuia wakimbizi wa Syria kurejea nchini kwao.

Sheikh Naim Qassim amesisitiza kuwa, Marekani na Umoja wa Ulaya zimekuwa zikichukua hatua mbalimbali za kuwazuia wakimbizi wa Syria kurejea nchini kwao..

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, lengo la Marekani na Umoja wa Ulaya la kuwazuia wakimbizi kurejea nchini Syria ni kutaka kuendesha propaganda kwamba, licha ya kuweko serikali katika nchi yao lakini raia hawawezi kuishi katika nchi hiyo.

Sheikh Naim Qassim ameeleza kuwa, kurejea wakimbizi nchini Syria maana yake ni kuwa, serikali ya Damascus imeweza kuiongoza nchi hiyo na kurejesha amani na usalama. 

Wakimbizi wa Syria

Syria ilitumbukia katika vita mwezi Machi 2011 ambapo Umoja wa Matiafa unasema hadi sasa 400,000 wameshauawa huku mamilioni ya wengine wakilazimikwa kuwa wakimbizi. Serikali ya Syria inalaumu baadhi ya nchi za Magharibi hasa Marekani na waitifakie wake katika eneo yaani Utawala wa Israel, Uturuki, Qatar na Saudi Arabia kuwa ndio waungaji mkono wakuu wa magaidi wakufurishaji nchini humo.

Wakati huo huo, jeshi la Syria limeendelea kuwaangamiza magaidi wanaopata himaya ya kigeni na limefanikiwa kuchukua udhibiti wa maeneo mengi yaliyokuwa yametekwa na kudhibitiwa na magaidi hao.

Tags