Wahajiri wa Kiarabu waandamana kupinga jinai za Saudia
Wahajiri Waarabu wamefanya maandamano katika mji mkuu wa Denmark, Copenhagen wakipinga jinai na uhalifu unaoendelea kufanywa na serikali ya Saudi Arabia katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati.
Waandamanaji hao wameashiria mwaka wa tano sasa wa kuwepo majeshi ya Saudia nchini Bahrain kwa ajili ya kukandamiza wananchi wanaodai haki zao za kimsingi na kutangaza uungaji mkono wao kwa raia wa nchi hiyo.
Vilevile wamelaani uvamizi na mauaji yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia na washirika wake huko Yemen na kusisitiza haki na mataifa ya Kiarabu ya kujiainishia mustakbali wao.
Kandokando ya maandamano hayo kulitayarishwa maonyesho ya picha zinazohusiana na jinai na mauaji ya kutisha yanayofanywa na Saudi Arabia katika nchi mbalimbali.
Waandamani Waarabi mjini Copenhagen pia wametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuichukilia hatua kali serikali ya Kifalme ya Riyadh kutokana na jinai na uhalifu wake katika nchi kadhaa jirani.
Maandamano hayo pia yamehudhuriwa na shakhsia mbalimbali za kutetea haki za binadamu.