Foreign Policy: Saudi Arabia inataka kutengeneza silaha za nyuklia
Jarida la Foreign Policy la Marekani limeripoti kuwa, Saudi Arabia inataka kutengeneza silaha za nyuklia ikishirikiana na Marekani.
Jarida la Foreign Policy limeashiria hati ya maelewano ya ushirikiano wa kinyuklia iliyotiwa saini na maafisa wa Saudi Arabia na Marekani na kuandika kuwa: Licha ya maafisa wa Saudia kukadhibisha suala hilo lakini inaonekana kuwa Riyadh ina malengo ya kutengeneza silaha za nyuklia.
Ripoti ya jarida hilo imengoza kuwa, katika hati hiyo Sadia ilipinga suala la kuwekewa mipaka katika urutubishaji wa madini ya urani na uzalishaji wa protanium, suala ambalo linaonesha kuwa, Riyadh imeazimia kutengeneza silaha za nyuklia.
Jarida la Foreign Policy limeandika kuwa: Saudi Arabia sio nchi nchi yenye utulivu wala inayopenda amani katika eneo la Mashariki ya Kati na kwa msingi huo haipasi kupewa mazingatio maalumu na serikali ya Marekani.

Limeongeza kuwa serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani inaoina Saudi Arabia kama mshirika wake lakini Wasaudia ndio waenezaji wa mfumo wa kifikra wa makundi ya kigaidi.
Jarida la Foreign Policy limesisitiza kuwa, Marekani haipaswi kuhadaiwa na mageuzi ya kimaonyesho tu ya mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia, Muhammad bin Salman kwa sababu serikali yake ni ya kidikteta na kiimla inayokandamiza wafuasi wa madhehebu za waliowachache na harakati za kisiasa za upinzani.