Imarati yakiri kwamba lilikuwa kosa kuiondoa Syria Arab League
Waziri wa Mambo ya Nje wa Imarati amekiri wazi kwamba maamuzi ya kuiondoa Syria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) yalikuwa makosa makubwa.
Anwar Gargash ameyasema hayo asubuhi ya leo na kuongeza kuwa, kuiondoa Syria katika jumuiya hiyo yalikuwa ni makosa na kukiri kwamba nchi za Kiarabu hazikutanishwi na malengo ya pamoja ya kisiasa. Kadhalika Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Imarati ameongeza kwamba nchi hizo za Kiarabu haziwezi kuwa na mpango wa pamoja kwa ajili ya utatuzi wa suala la Syria. Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kupitia mashinikizo mbalimbali ya nchi za Magharibi ilitangaza ksimamisha uanachama wa Syria katika jumuiya hiyo mwezi Novemba 2011.
Mgogoro wa Syria uliibuka kuanzia mwaka 2011 baada ya makundi ya kigaidi na ukufurishaji yanayopata uungaji mkono wa kifedha na sila kutoka Saudia, Imarati, Marekani na waitifaki wao kutumwa ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu kwa lengo la kuleta mabadiliko ya mlingano katika eneo kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni. Mahusiano ya karibu ya baadhi ya watawala wa Kiarabu wakiwemo viongozi wa Saudia na Imarati na utawala wa Kizayuni, yamepelekea kushadidi mgogoro katika eneo la magharibi mwa Asia ikiwemo Syria, Iraq na Yemen.