Uwezo na mafanikio ya Iran vyamkosesha utulivu Netanyahu
Suala la Iran limekuwa likizidi kuvuruga akili ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala Haramu wa Israel kiasi kwamba hata katika nyakati za mapumziko kadhia ya Iran inamkosesha utulivu.
Gazeti la Kizayuni la Jerusalem Post limeandika kuwa, picha zilizochukuliwa na kamera maalumu za kufuatilia usalama wa ndani, zinaonyesha kwamba hata katika nyakati za mapumziko, Netanyahu huwa anashughulishwa sana na suala la Iran. Gazeti hilo limeongeza kwamba, moja ya picha za kamera hizo inaomunyesha waziri mkuu huyo mkuu wa utawala katili wa Israel akisoma makala zinazoihusu Iran ndani ya nyakati wa mapumziko, huku akishirikiana na Yisrael Katz, Waziri wa Upelelezi wa utawala huo.
Hii ni katika hali ambayo siku za nyuma, Netanyahu alijulikana kwa kusoma vitabu zinavyozungumzia maisha ya Winston Churchill, Waziri Mkuu wa Zamani wa Uingereza. Suala hilo linaonyesha kwamba, sasa Netanyahu amepatwa na khofu kubwa kutokana na nguvu kubwa ya Iran katika eneo la Mashariki ya Kati kiasi kwamba hata safari za viongozi kadhaa wa ngazi ya juu wa Marekani huko Tel Aviv, hazijaweza kumpunguzia wasiwasi na wahka mkubwa alionao Netanyahu kutokana na Iran.