Makumi ya walowezi wa Kizayuni wavamia Msikiti wa al-Aqswa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i49154-makumi_ya_walowezi_wa_kizayuni_wavamia_msikiti_wa_al_aqswa
Makumi ya walowezi wa Kizayuni wamevamia Msikiti wa al-Aqswa wakiwa wanasaidiwa na askari wa jeshi la utawala haramu wa Israel na kufanya vitendo vya kuuvunjia heshima msikiti huo mtakatifu.
(last modified 2025-11-07T07:21:00+00:00 )
Oct 31, 2018 08:16 UTC
  • Makumi ya walowezi wa Kizayuni wavamia Msikiti wa al-Aqswa

Makumi ya walowezi wa Kizayuni wamevamia Msikiti wa al-Aqswa wakiwa wanasaidiwa na askari wa jeshi la utawala haramu wa Israel na kufanya vitendo vya kuuvunjia heshima msikiti huo mtakatifu.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, walowezi hao wa Kizayuni baada ya kuingia katika eneo la ndani la msikiti huuo  walisikika wakipiga nara dhidi ya Uislamu.

Duru za Palestina zinasema kuwa, polisi ya utawala wa Kizayuni wa Israel iliandaa mazingira ya kiusalama kwa ajili ya kuingia katika eneo hilo walowezi hao wa Kizayuni.  

Ripoti zaidi zinasema kuwa, hujuma na uvamizi wa walowezi wa Kizayuni katika Msikiti wa al-Aqswa umeongezeka mno katika siku za hivi karibuni. 

Askari wa Kizayuni wakiuvamia Msikiti wa al-Aqswa

Inaelezwa kuwa, karibu kila siku walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakifanya uvamizi katika msikiti huo lengo likiwa ni kutekeleza njama za kutokomeza utambulisho wa Kiislamu na Kikristo wa Msikiti wa al-Aqswa na badala yake kuweka nembo za Kizayuni.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya juhudi za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Hata hivyo kusimama kidete wananchi wa Palestina hadi sasa kumekwamisha njama na mipango yote ya Wazayuni, zikiwemo njama za kutaka kubadilisha muundo wa kijamii na kijiografia wa Baytul Muqaddas.