Marekani yaendeleza umwagaji damu Syria, yaua watu 8 wa familia moja
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i50022-marekani_yaendeleza_umwagaji_damu_syria_yaua_watu_8_wa_familia_moja
Muungano wa eti kupambana na magaidi wa Daesh unaoongozwa na Marekani umeendelea kufanya mashambulizi yake ya anga katika mkoa wa mashariki wa Deir ez-Zor nchini Syria na kuua raia wengi.
(last modified 2026-04-28T05:09:17+00:00 )
Dec 07, 2018 20:55 UTC
  • Marekani yaendeleza umwagaji damu Syria, yaua watu 8 wa familia moja

Muungano wa eti kupambana na magaidi wa Daesh unaoongozwa na Marekani umeendelea kufanya mashambulizi yake ya anga katika mkoa wa mashariki wa Deir ez-Zor nchini Syria na kuua raia wengi.

Duru za kuaminika zimeliambia shirika la habari la SANA kuwa, raia wasiopungua wanane waliuawa jana Ijumaa, baada ya ndege hizo za kivita za US kufanya hujuma katika mji wa Hajin, kusini mwa mkoa huo.

Habari zaidi zinasema kuwa, watu waliouwa katika shambulizi hilo la jana la anga ni wa familia moja. 

Mauaji ya jana yanajiri siku mbili baada ya watu wengine watano kuuawa katika shambulizi jingine la anga la ndege za kivita za Marekani katika mji huo huo wa Hajin.

Sehemu ya hujuma za anga za Marekani nchini Syria

Aidha mwishoni mwa mwezi uliopita, raia 20 wa Syria wakiwemo watoto wadogo na wanawake waliuawa katika shambulizi jingine la anga lililofanywa na ndege za muungano vamizi dhidi ya mji wa Hajin, mkoani Dayr al-Zawr, mashariki mwa nchi.

Hadi hivi sasa muungano vamizi wa kijeshi wa Marekani umeshaua idadi kubwa ya wananchi wasio na hatia wa Syria na Iraq, tangu uundwe mwaka 2014.