Jeshi la Syria laangamiza maficho ya magaidi wa Jabhat al Nusra mkoani Hama
(last modified Tue, 19 Mar 2019 15:03:21 GMT )
Mar 19, 2019 15:03 UTC
  • Jeshi la Syria laangamiza maficho ya magaidi wa Jabhat al Nusra mkoani Hama

Wanajeshi wa Syria wameshambulia na kuangamiza maficho ya magaidi wa Jabhat al Nusra katika viunga vya mkoa wa Hama wa magharibi mwa nchi hiyo.

Televisheni ya al Alam imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, katika operesheni hiyo jeshi la Syria limeshambulia maficho ya genge la ukufurishaji la Jabhat al Nusra katika mlima wa Shashabo kwenye viunga vya kaskazini mwa mkoa wa Hama na kuangamiza magaidi kadhaa.

Baadhi ya magenge ya kigaidi yanatumia maeneo ya mbali ya kaskazini mwa mkoa wa Hama na mkoa wa Idlib kufanya mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Syria hivyo jeshi hilo limelazimika kujibu mashambulizi ya magaidi hao.

Wakati huo huo gazeti la al Quds al Arabi limezinukuu duru za wapinzani wa Syria zikisema kuwa, baadhi ya wapigaji wa Peshmerga wa eneo la Kurdistan ya Iraq wamepelekwa katika viunga vya mashariki vya mkoa wa Deir ez-Zor  huko mashariki mwa Syria.

Magaidi wa Jabhat al Nusra wanaoungwa mkono na Israel na Marekani nchini Syria

 

Jasema al Muhammad, mmoja wa wanaharakati wa kisiasa nchini Syria amesema kuwa wapiganaji wa Peshmerga wa Kurdistan ya Iraq wamepelekwa mashariki mwa Mto Furat kama sehemu ya mpango wa Marekani wa kujizatiti kinyume cha sheria katika ardhi hiyo ya Syria.

Ingawa rais wa Marekani, Donald Trump, amekuwa akidai mbele ya vyombo vya habari kuwa ana nia ya kuondoa wanajeshi wake nchini Syria, lakini kila leo anazidi kujizatiti kinyume cha sheria katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Tags