Daesh inafanya biashara ya kuuza figo za binadamu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i550-daesh_inafanya_biashara_ya_kuuza_figo_za_binadamu
Katika kuendeleza jinai zake dhidi ya binadamu, kundi la kigaidi la Daesh linafanya biashara ya kuuza figo za binadamu katika maeneo inayoyadhibiti.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 04, 2016 03:29 UTC
  • Daesh inafanya biashara ya kuuza figo za binadamu

Katika kuendeleza jinai zake dhidi ya binadamu, kundi la kigaidi la Daesh linafanya biashara ya kuuza figo za binadamu katika maeneo inayoyadhibiti.

Duru za kuaminika katika mji wa Mosul nchini Iraq zimeripotii kuwa, hospitali za mji huo hivi sasa zinanunua figo kwa bei ya dinari milioni tano sawa na karibu dola 4200 kwa amri ya Daesh na kisha huziuza kwa wahitaji kwa bei mara tatu zaidi.

Duru hizo zimesisitiza kuwa wakazi wengi wa mji wa Mosul wanauza figo zao kutokana na kuhitajia fedha na hadi sasa visa 126 vimeripotiwa katika hospitali kuu ya mji huo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kundi la kigaidi la Daesh linatumia vibaya matatizo ya kiuchumi ya wananchi na kuwauzia watu figo za wananchi hao kwa bei i mara tatu zaidi. Huko nyuma pia duru za kimataifa ziliwahi kutoa ripoti juu ya mahusiano yaliyopo kati ya kundi la kigaidi la Daesh na madalali wa kimataifa na bishara ya magendo ya binadamu kati ya pande hizo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, tangu mwaka jana kundi la kigaidi la Daesh lilianza kazi rasmi ya kuuza viungo vya binadamu baada ya kubadili moja ya ikulu za Saddam Hussein, dikteta wa zamani wa Iraq huko Musul na kuwa hospitali maalumu.