Palestina: Utawala haramu wa Israel unatekeleza mipango yake ya kikoloni
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imelaani vikali hatua za jeshi la utawala haramu wa Israel za kuendelea kubomoa nyumba na makazi ya Wapalestina.
Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeeleza kwamba, Wazayuni wanatekeleza mipango ya kikoloni ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.
Sehemu nyingine ya taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeitaka jamiii ya kimataifa kuchukua hatua za kivitendo za kukabiliana na ubomoaji wa nyumba za Wapalestina unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu hususan huko Quds na viunga vyake.
Taarifa hiyo imeutaka Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama, Baraza la Haki za Binadamu na Mahakama aya Kimataifa ya Jinai kusitisha jinai hizo na kwamba, zifahamu kwamba, zina jukumu la kisheria na kimaadili kuhusiana na suala hilo.
Desemba 23, 2016 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio 2334 ambalo liliutaka utawala haramu wa Israel usimamishe haraka na kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa vitongoji katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.
Utawala wa Kizayuni ambao unaungwa mkono kikamilifu na Marekani katika hatua zake hizo haramu umedhamiria kubadilisha muundo wa kijiografia na kidemografia wa maeneo ya Palestina; ili kwa kuyazayunisha maeneo hayo, kuhakikisha unazihodhi na kuzidhibiti kikamilifu ardhi za Wapalestina.