Damascus: OPCW ni genge la kuwahami wahalifu na magaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i69310-damascus_opcw_ni_genge_la_kuwahami_wahalifu_na_magaidi
Wizara ya Mambo ya Nchi za Mje wa Syria imelaani uamuzi uliotolewa dhidi ya nchi hiyo na Shirika la Kimataifa la Kuzuia Matumizi ya Silaha za Kemikali, (OPCW) ambao rasimu yake imetayarishwa na Ufaransa na kuutaja kuwa unayaunga mkono na kuyahami makundi ya kigaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 22, 2021 02:32 UTC
  • Damascus: OPCW ni genge la kuwahami wahalifu na magaidi

Wizara ya Mambo ya Nchi za Mje wa Syria imelaani uamuzi uliotolewa dhidi ya nchi hiyo na Shirika la Kimataifa la Kuzuia Matumizi ya Silaha za Kemikali, (OPCW) ambao rasimu yake imetayarishwa na Ufaransa na kuutaja kuwa unayaunga mkono na kuyahami makundi ya kigaidi.

Taaarita ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Syria imelaani vikali azimio hilo la nchi za Magharibi lililotolewa katika mkutano wa 25 wa nchi wanachama katika Shirika la Kimataifa la Kuzuia Matumizi ya Silaha za Kemikali (OPCW) dhidi ya Syria na kusisitiza kuwa, hilo ni tukio hatari katika utendaji wa shirika hilo na kwamba halioani na hati ya OPCW.

Jumatano ya jana Shirika la Kimataifa la Kuzuia Matumizi ya Silaha za Kemikali lilisimamisha haki za Syria katika shirika hilo ikiwa ni pamoja na haki ya kupiga kura kwa kisingizio kwamba, mwezi Machi mwaka 2017 ilitumia silaha za kemikali katika eneo la al Lataminah huko kaskazini mwa nchi hiyo na huko Saraqib mwaka 2018.

Muswada wa azimio hilo ambalo ndilo la kwanza la aina hii kutolewa na OPCW ulitayarishwa na Ufaransa na kuungwa mkono na nchi 87. Nchi nyingine 15 zimelipinga na 34 zimejizuia kupiga kura. 

Taarifa ya serikali ya Damascus imesema, azimio hilo ni katika fremu ya kuyahama na kuyaunga mkono makundi ya kigaidi na kwamba, kwa hatua hiyo, nchi za Magharibi zinayahamasisha makundi ya kigaidi kuendelea kufanya jinai na uhalifu ikiwa ni pamoja na kutumia silaha za kemikali.

Ni vyema kukumbusha hapa kuwa, wapinzani wa serikali ya Syria na wafadhili wao wa Kimagharibi na Kiarabu wameshindwa katika medani ya vita, mara kadhaa wamekuwa wakitumia mbinu za kuibua tuhuma, kutoa madai ya uongo na kutumia vibaya taasisi za kimataifa. Moja ya mbinu hizo ni kuituhumu serikali ya Syria kuwa imetumia silaha za kemikali dhidi ya wapinzani na raia wa nchi hiyo.