HAMAS yawapa mbinu Wapalestina wa Quds za kupambana na Wazayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i70538-hamas_yawapa_mbinu_wapalestina_wa_quds_za_kupambana_na_wazayuni
Mjumbe mwandamizi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amewataka Wapalestina wanaoishi katika mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas kutotulia, bali waendelee kujibu jinai zote zinazofanywa na wanajeshi wa Israel na walowezi wa Kizayuni dhidi yao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 25, 2021 06:35 UTC
  • HAMAS yawapa mbinu Wapalestina wa Quds za kupambana na Wazayuni

Mjumbe mwandamizi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amewataka Wapalestina wanaoishi katika mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas kutotulia, bali waendelee kujibu jinai zote zinazofanywa na wanajeshi wa Israel na walowezi wa Kizayuni dhidi yao.

Shirika la habari la FARS limeripoti habari hiyo leo na kumnukuu Dk. Mousa Abumarzook, kiongozi mwandamizi wa HAMAS akisema kwenye mtandao wa kijamii wa Twotter kwamba, ukumbi wa al Buraq ni katika sehemu kuu za Msikiti mtakatifu wa al Aqsa. Ni katika eneo hilo ndipo ilipo misikiti miwili muhimu ya al Maghariba na al Buraq. Kusimama imara watu wetu huko Quds na maeneo mengine ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, katika kukilinda na kukitetea Kibla cha Kwanza cha Waislamu na eneo la miiraji na safari ya kwenda mbinguni Bwana Mtume Muhammad SAW ni neema isiyo na kifani na ni fakhari kubwa kwetu. Hivyo ni wajibu kuulinda ukumbi wa al Buraq na kuendelea kutekelezwa ibada za Waislamu katika eneo hilo, na hayo ndiyo majibu bora kabisa kwa Wazayuni.

Wazayuni maghasibu wanafanya jinai kubwa dhidi ya Kibla cha Kwanza cha Waislamu

 

Utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia vibaya mghafala wa jamii ya kimataifa na unazidi kuchimba mashimo katika eneo hilo la al Buraq lenye misikiti ya Waislamu ikiwa ni kuendeleza mradi wa Wazayuni wa kujenga hekalu la Solomon.

Kabla ya hapo pia, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilikuwa imewatahadharisha Wazayuni maghasibu wasifanye chokochoko na mashambulizi ya aina yoyote dhidi ya Quds na Msikiti Mtukufu wa al Aqsa.

Juzi Jumapili na ikiwa imepita siku mbili tu baada ya kutangazwa usitishaji vita kati ya wanamuqawama na utawala wa Kizayuni, wanajeshi na walowezi wa Kizayuni waliuvamia msikiti wa al Aqsa na kusababisha mapigano makali kati ya raia wa Palestina na wanajeshi wa utawala huo ghasibu.