Saudia yalegeza msimamo mkali na kurejesha balozi wake Doha, Qatar
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i71528-saudia_yalegeza_msimamo_mkali_na_kurejesha_balozi_wake_doha_qatar
Utawala wa Saudi Arabia umelegeza misiammo yake mikali na hatimaye kuafiki kumrejesha balozi wake katika mji mkuu wa Qatar, Doha, baada ya miaka minne.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 21, 2021 23:50 UTC
  • Saudia yalegeza msimamo mkali na kurejesha balozi wake Doha, Qatar

Utawala wa Saudi Arabia umelegeza misiammo yake mikali na hatimaye kuafiki kumrejesha balozi wake katika mji mkuu wa Qatar, Doha, baada ya miaka minne.

Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Qatar, QNA, jana Jumatatu Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar alipokea vitambulisho vya balozi mpya wa Saudi Arabia ambaye ambaye amewasilisha vitambulisho vyake.

Balozi mpya wa Saudi Arabia nchini Qatar Mwanamfalme Mansour bin Khalid bin Farhan Al-Saud alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar  Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani na kumkabidhi vitambulisheo vyake.

Katika kikao hicho, Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar aliahidi kuchukua hatua ili kuimarisha uhusianoo wa nchi mbili.

Khalid bin Farhan Al-Saud aliwaku kuwa balozi wa Saudi Arabia nchini Uhusiano. 

Ikumbukwe kuwa, Saudi Arabia, Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), nchi tatu ambazo ni wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi, pamoja na Misri, mnamo Juni 5 mwaka 2017 ziliituhumu Qatar kuwa inaunga mkono ugaidi na zikakata uhusiano wao na nchi hiyo. Aidha nchi hizo nne zilifunga mipaka yao na Qatar baharini, angani na nchi kavu.

Saudi Arabia na nchi hizo tatu zilitangaza masharti 13 ambayo Qatar ilipaswa kuyatimiza kabla ya uhusiano kurejea lakini Qatar imesema masharti hayo yanakiuka mamlaka yake ya kujitawala na imekataa kuyatekeleza.

Baada ya kushindwa Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka 2020, Saudi Arabia ilipunguza shari na kuanza kuchukua mkondo wa kutaka kuboresha uhusiano wake na Qatar.  Baada ya Qatar kukataa kutii masharti ya Saudia wakuu wa Riyadh hawakuwa na budi ila kulegeza msimamo na kuanzisha tena uhusiano na Doha.