Umoja wa Mataifa watahadharisha kuhusu tatizo kubwa wa chakula nchini Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i74190-umoja_wa_mataifa_watahadharisha_kuhusu_tatizo_kubwa_wa_chakula_nchini_afghanistan
Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusiana na uhaba mkubwa chakula nchini Afghanistan na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka za kuisaidia nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 02, 2021 07:27 UTC
  • Umoja wa Mataifa watahadharisha kuhusu tatizo kubwa wa chakula nchini Afghanistan

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusiana na uhaba mkubwa chakula nchini Afghanistan na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka za kuisaidia nchi hiyo.

Ramiz Alakbarov, mratibu wa kieneo wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan amesema kuwa, theluthi moja ya wakazi milioni 38 nchini humo wanakabiliwa na hali ya dharura au mgogoro wa usalama wa chakula.

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amebainisha kwamba, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, (WFP) katikak majuma ya hivi karibuni limewagawia chakula makumi ya maelfu ya wananchi wa Afghanistan. Aidha amesema kuwa, ni asilimia 39 ya kiasi cha fedha dola milioni 1.3 kinachohitajika ndicho ambacho hadi sasa kimepatikana kwa ajili ya misaada ya wananchi wa Afghanistan.

Wakimbizi wa Afghanistan

 

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, hivi sasa nusu ya wananchi wa Afghanistan wanahitajia misaada ya kibinadamu ili waweze kuendelea kuishi na kkwamba, Afghanistan inakaribia kutumbukia katika janga la kibinadamu.

Jumapili tarehe 15 mwezi uliopita wa Agosti serikali ya Rais Muhammad Ashraf Ghani ilisambaratika na kiongozi huyo kuikimbia nchi baada ya Taliban kuingia Kabul mji mkuu wa Afghanistan. Wachambuzi wa mambo wanasema, hatua ya wanamgambo wa Taliban ya kuudhibiti mji wa Kabul imehitimisha uvamizi wa miaka 20 wa Marekani na nchi nyingine za Magharibi kwa kisingizio cha kuijenga upya Afghanistan.