Vyombo vya Kizayuni vyakiri kufeli Israel Ukanda wa Ghaza
(last modified Sat, 11 Sep 2021 01:30:06 GMT )
Sep 11, 2021 01:30 UTC
  • Vyombo vya Kizayuni vyakiri kufeli Israel Ukanda wa Ghaza

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimekiri kushindwa Israel katika vita vya hivi karibuni vya Ukanda wa Ghaza na kusema kuwa, kiwango cha kufeli huko ni kikubwa sana.

Vyombo hivyo vya habari vya Kizayuni vimewahoji wataalamu wengi wa Israel na wamekiri kuwa jeshi la utawala wa Kizayuni lilishindwa vibaya katika vita vya hivi karibuni vya Ukanda wa Ghaza. Wataalamu hao wamesema, Israel imepoteza kikamilifu udhibiti wa ukanda huo.

Yuni Ben Menachem, afisa wa zamani wa shirika la ujasusi wa jeshi la utawala wa Kizayuni ni mmoja wa wataalamu hao Wazayuni aliyehojiwa na vyombo vya habari vya Israel. Amegusia namna Mpalestina mmoja alivyomfyatulia risasi askari Mzayuni kwenye Ukanda wa Ghaza na kusema, inabidi askari wa Israel wapewe amri ya kijeshi ya kupimga risasi mtu yeyote anayeukaribia ukuta wa kuyazingira maeneo ya Wapalestina.

Wazayuni walifanya mashambulizi ya kiholela dhidi ya raia baada ya kushindwa kukabiliana na wanamuqawama wa Palestina

 

Afisa huyo mstaafu wa shirika la kijasusi la Israel pia amewataka waziri wa vita wa utawala huo katili, Benny Gantz na mkuu wa jeshi la utawala wa Kizayuni, Aviv Kochavi watumie mabavu na nguvu zaidi kukabiliana na muqawama wa Wapalestina. Askari mmoja Mzayuni alijeruhiwa vibaya Jumamosi iliyopita wakati Wapalestina walipoitisha maandamano ya "Siku ya Hasira."

Jumapili asubuhi ndege za utawala wa Kizayuni zilishambulia kwa mabomu maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Ghaza, mashambulizi ambayo yalijibiwa kwa mvua ya makombora na wanamapambano wa Palestina.

Utawala wa Kizayuni umeizingira Ghaza tangu mwaka 2006 hadi hivi sasa kwa kuifungia njia zote za kuingia na kutoka kwenye eneo hilo, lakini Wapalestina wamezidi kuwa imara tofauti na ndoto za Wazayuni.

Tags