Mossad inakula njama ya kuzuia kufufuliwa JCPOA
Mkuu wa Shirika la Kijasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel (Mossad) anatazamiwa kuelekea Washington kufanya mikutano kadhaa ya faragha na maafisa wa serikali ya Marekani kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
Duru za habari katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Yair Lapid zimesema, mkuu huyo wa Mossad anaelekea Washington kwa ajili ya kushawishi viongozi wa serikali ya Rais Joe Biden wasiidhinishe makubaliano ya kuhuisha JCPOA.
Tel Aviv inadai kuwa, iwapo mapatano hayo ya mwaka 2015 yatafufuliwa na Marekani irejee kwayo, Tehran itazalisha silaha za nyuklia, mbali na kuweza kuyahami makundi eti yanayopigana kwa niaba ya Iran katika eneo.
Siku chache zilizopita, Naftali Bennett, Waziri Mkuu wa Israel alidai kuwa, kupasishwa kwa mapatano hayo kutaipa serikal ya Iran robo ya dola trilioni moja, fedha ambazo zitaiwezesha Tehran kuzalisha, kusimika na kuendesha mitambo ya mashinepewa pasi na kizuizi kwa miaka miwili.
Hii ni katika hali ambayo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza mara chungu nzima kuwa haina azma wala nia ya kuunda silaya za nyuklia, kwani huko ni kwenda kinyume na sera za Jamhuri ya Kiislamu.
Utawala huo haramu unaibua madai dhidi ya Iran katika hali ambayo, wenye una miliki vichwa vya silaha za atomiki visivyopungua 300.