Wasiwasi wa Israeli kuhusu matukio mapya ya kimkakati katika Asia Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i96590-wasiwasi_wa_israeli_kuhusu_matukio_mapya_ya_kimkakati_katika_asia_magharibi
Katika wiki za hivi karibuni, kumekuwapo matukio kadhaa ya kimkakati katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) ambayo yameufanya utawala wa Kizayuni wa Israel uingiwe na wasiwasi na hofu kubwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 23, 2023 13:03 UTC
  • Benjamin Netanyahu
    Benjamin Netanyahu

Katika wiki za hivi karibuni, kumekuwapo matukio kadhaa ya kimkakati katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) ambayo yameufanya utawala wa Kizayuni wa Israel uingiwe na wasiwasi na hofu kubwa.

Kwanza ni mshikamano ambao uliibuka kati ya pande tofauti za mhimili wa muqawama au mapambano. Huu ni mshikamano ambao ulidhihirika baada ya mashambulio ya hivi karibuni ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al –Aqsa. Makundi ya muqawama huko Palestina na Lebanon yalijibu jinai hiyo kwa mashambulizi ya pamoja dhidi ya Israel.

Yoav Gallant Waziri wa Vita vya Utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kwamba utawala huo sasa unakabiliwa na changamoto mpya kutoka kwa harakati za muqawama.

Matamshi hayo yametolewa baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutangaza kuanguka kwa moja ya ndege zake zisizo na rubani wakati wa uvamizi wa anga ya Syria.

Kwa mujibu wa gazeti la Israel "Yadiyot Aharanot", msemaji wa jeshi la Israel alidai Jumatano iliyopita kwamba ndege ya jeshi la utawala huo ilianguka katika eneo la Syria wakati ilipokuwa ikiruka katika anga ya nchi hiyo Jumanne usiku. Ben Kinon alisema kuwa chanzo cha suala hilo kinachunguzwa na amejiepusha kutaja aina ya ndege isiyo na rubani iliyoanguka nchini Syria na kudai kuwa hakuna hatari ya kuvuja kwa taarifa za ndege hiyo isiyo na rubani.

Kabla ya hapo msemaji wa jeshi la Kizayuni alikuwa ametangaza habari ya kutunguliwa ndege nyingine isiyo na rubani ya utawala huo katika anga ya Syria.

Inavyoelekea ni kuwa hivi sasa ndege zisizo na rubani za Israel zinatunguliwa mara kwa mara nchini Syria zaidi ya huko nyuma. Hivyo inaonekena kwamba Syria iko tayari kutoa pigo kwa utawala wa Kizayuni.

Syria imefanikiwa kuvuka kwa mafanikio njama ya kuangusha serikali yake ingawa imepata hasara ya kuuawa makumi ya maelfu ya watu na pia hasara ya mabilioni ya dola. Hivi sasa  nchi hiyo inajenga upya jeshi lake kwa msaada wa Iran na Russia na imeweza kuimarisha uwezo wake wa kujihami angani.

Aidha madola yote ya kieneo yaliyokuwa yakiunga mkono vikundi vya waasi au magaidi wakufurishaji sasa yamebadilika moja baada ya nyingine. Hivi sasa madola hayo yanataka maridhiano na serikali kuu ya Damascus na yako mbioni kuanzisha tena uhusiano na Syria.

Miongoni mwa pande za mhimili wa muqawama ni Syria pekee ambayo hadi sasa imekuwa ikichukua tahadhari na kujizuia kuingia katika makabiliano ya moja kwa moja ya kijeshi na Israel lakini sasa inaonekana kwamba, Damascus, ksms zilivyo pande zingine za muqawama, imechukua hatua ya kuimarisha uwezo wa kumzuia adui Mzayuni.

Tukio jingine katika ‘Mhimili wa Muqawama’  ni kuhusu baadhi ya nchi za Kiarabu ambazo hapo awali zilikuwa waitifaki sugu wa Marekani na utawala wa Kizayuni katika makabiliano na ‘Mhimili wa Muqawama’ ambazo sasa zimebadili sera na kuanza kurejesha uhusiano wa kawaida na Iran.

Hivi karibuni, Iran ambayo ni nguzo muhimu katika ‘Mhimili wa Muqawama’ ilitiliana saini mapatano na Saudi Arabia kuhusua kuanza tena uhusiano wao wa kidiplomasia, mapatano hayo yalitiwa saini Machi 10 mwezi uliopita kwa upatanishi wa Beijing.

Kufuatia makubaliano hayo, Saudi Arabia ilimwalika Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Feisal Miqdad, ikiwa ni hatua ya kuirejesha Syria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu. Safari hiyo ilifuatiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia, Faisal Bin Farhan, kwenda Damascus na kukutana na Rais Bashar Al –Assad wa Syria.

Faisal Bin Farhan akizungumza na Rais Bashar Assad wa Syria

Kwa upande mwingine, katika Ghuba ya Uajemi, Iran iliteua balozi wake Abu Dhabi baada ya miaka mingi ya mvutano na Umoja wa Falme za Kiarabu. Sambamba na matukio haya, Qatar na Bahrain zimerejesha tena uhusiano wa kidiplomasia kati yao. Zaidi ya hayo, ujumbe kutoka Hamas, ulioongozwa na Ismail Haniyeh na Khaled Mashal, ulikwenda Saudi Arabia baada ya miaka 15 ya kuvunjika uhusiano wa Hamas na Riyadh.

Utawala wa Wazayuni na baadhi ya tawala za Kiarabu zimekuwa na msimamo wa pamoja kuhusu mgogoro wa Syria kwa miaka 12 iliyopita.

Pande zote mbili zilitaka kupinduliwa serikali ya Bashar al -Assad, na hata zilipanga njama ya kuigawa Syria ili kudhoofisha Mhimili wa Muqawama katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Lakini sasa ukaribu na uboreshaji wa uhusiano wa Syria na nchi za Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi sambamba na makubaliano ya Iran na Saudia, halikadhalika kuboreka uhusiano wa Saudia na Hamas ni mambo ambayo yameibua wasiwasi katika utawala wa Kizayuni na kuvuruga ndoto ya utawala huo ya kuunda muungano wa kimataifa dhidi ya Iran.

Gazeti la Kizayuni la Ma'ariv limekuetaja kurudi Syria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuwa ni "Mashariki ya Kati Mpya". Kuimarika uwezo wa kijeshi wa pande zote za ‘Mhimili wa Muqawama’ ni nukta ya mwisho ambayo imeutia kiwewe utawala wa Kizayuni.