Wananchi wa Jordan waandamana kuunga mkono muqawama wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i99150-wananchi_wa_jordan_waandamana_kuunga_mkono_muqawama_wa_palestina
Maelfu ya wananchi wa Jordan wameandamana kwa ajili ya kuunga mkono muqawama na mapambano ya wananchi wa Palestina na wakati huo huo kulaani jinai za kila leo za utawala haramu wa Israel.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Jun 24, 2023 04:28 UTC
  • Wananchi wa Jordan waandamana kuunga mkono muqawama wa Palestina

Maelfu ya wananchi wa Jordan wameandamana kwa ajili ya kuunga mkono muqawama na mapambano ya wananchi wa Palestina na wakati huo huo kulaani jinai za kila leo za utawala haramu wa Israel.

Maandamano hayo yaliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Amman yamehudhuriwa na matabaka mbalimbali ya wananchi.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walisikika wakipiga nara dhidi ya utawala haramu wa Kizayunii wa Israel unaotenda jinai kila uchao huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Kwa mujibu wa tovuti ya "Al Arabi Al-Jadeed", washiriki wa maandamano hayo wametaka serikali ya Jordan kufuta mikataba yote iliyotiwa saini na utawala huo ghasibu na kulaani kimya cha nchi za Kiarabu dhidi ya jinai za utawala huo ghasibu katika ardhi za Palestina.

Waandamanaji hao pia wamesisitiza haja ya kuchukuliwa hatua za haraka za kuliunga mkono taifa la Palestina na muqawama wake wa kishujaa.

Israel imeendelea kufanya mauaji kila uchao huko Palestina huku Umoja wa Mataifa na baraza lake la Usalama zikishindwa kuchukua hatua za maana kukomesha mauaji hayo

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anakosolewa vikali na mashirika ya kutetea haki za binadamu kwa kutoliweka jina la utawala haramu wa Israel kwenye orodha ya tawala wauaji wa watoto.

Mashirika hayo yamesema ni kosa na aibu kubwa kwa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutoliweka jina la Israel kwenye orodha hiyo inayofahamika kama 'Orodha ya Fedheha' ya Umoja wa Mataifa, licha ya utawala huo wa Kizayuni kuua makumi ya watoto wa Kipalestina mwaka jana na kuendelea kufanya hivyo tangu kuanza mwaka huu (2023).