-
Hitilafu kubwa baina ya Riyadh na Abu Dhabi kuhusu uongozi wa Ulimwengu wa Kiarabu
Jul 20, 2023 08:34Katika ripoti yake ya karibuni, jarida la Wall Street Journal linalochapishwa Marekani limeashiria hitilafu kubwa za kimitazamo zilizopo kati ya Mohammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia, na Mohammad bin Zayed, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati); na kuandika kuwa: Mgogoro huo, ambao dalili zake zilionekana kitambo nyuma, ulibainika hadharani Disemba mwaka uliopita.
-
Hamas yalaani uamuzi wa Marekani unaoitambua Israel kama "nchi isiyo na ubaguzi wa rangi"
Jul 20, 2023 08:13Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani hatua ya Kongresi ya Marekani ya kupasisha azimio linaloitaja Israel kuwa "taifa lisilo la kibaguzi", na kusema kuwa uamuzi huo ni upendeleo wa wazi wa Marekani kkwa uvamizi huo na unaihimiza Israel kuendeleza jinai na uhalifu wake dhidi ya watu wa Palestina.
-
Marekani yaziwekea vikwazo benki 14 za Iraq kwa kushirikiana na Iran
Jul 20, 2023 04:33Marekani imetangaza kuziwekea vikwazo benki 14 za Iraq kwa tuhuma za kushirikiana na Iran.
-
Kuvunjiwa heshima Qurani; Wairaq waushambulia ubalozi wa Sweden
Jul 20, 2023 04:03Wananchi wa Iraq waliokuwa na ghadhabu wameuvamia ubalozi wa Sweden mjini Baghdad na kuchoma moto sehemu moja ya ofisi za ubalozi huo, kulalamikia kibali cha pili kilichotolewa na serikali ya Stockholm cha kuruhusu kuvunjiwa heshima Qurani Tukufu katika nchi hiyo ya Ulaya.
-
ICC kuruhusu Wapalestina mtandaoni kuwashtaki Wazayuni kwa jinai za kivita
Jul 19, 2023 06:07Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inatazamiwa kuzindua jukwaa la mtandaoni litakalowawezesha wananchi wa Palestina kuwashtaki Wazayuni kwa jinai za kivita mbele ya taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa.
-
Mamilioni ya watoto wa Yemen wanakabiliwa na hatari ya baa la njaa
Jul 19, 2023 04:30Zaidi ya watoto milioni 6 nchini Yemen wanakabiliwa na hatari ya baa la njaa na kwamba, wanahitajia misaada ya haraka ya chakula na dawa.
-
Maandamano ya wapinzani wa mageuzi ya mahakama yazidi kuiteteresha serikali ya Netanyahu
Jul 19, 2023 04:30Wapinzani wa mpango wa Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel wa kufanyia mageuzi mfumo wa mahakama wameendelea kuandamana na kuzidi kutishia uhai wa serikali ya Netanyahu na washirika wake.
-
Malengo ya safari ya Erdogan nchini Saudi Arabia
Jul 19, 2023 03:32Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ameitembelea Saudi Arabia huku akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa kisiasa na kiuchumi wa nchi yake. Akiwa katika hatua ya kwanza ya safari yake ya siku tatu katika nchi kadhaa za Ghuba ya Uajemi, Erdogan aliwasili Jeddah, Saudi Arabia Jumatatu Julai 17.
-
Nasrullah: Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran lilikuwa tukio la karne
Jul 19, 2023 00:27Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran lilikuwa tukio kubwa zaidi katika karne iliyopita.
-
Wanamuqawama watekeleza oparesheni 20 dhidi ya Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi
Jul 18, 2023 08:12Duru za habari za Palestina zimetangaza kuwa, wanamapambano wa Palestina jana walitekeleza oparesheni 20 za kimuqawama dhidi ya Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na huko Quds inayokaliwa kwa mabavu.