Jul 19, 2023 09:37 UTC
  • ICC kuruhusu Wapalestina mtandaoni kuwashtaki Wazayuni kwa jinai za kivita

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inatazamiwa kuzindua jukwaa la mtandaoni litakalowawezesha wananchi wa Palestina kuwashtaki Wazayuni kwa jinai za kivita mbele ya taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa.

Hayo yamesemwa na Omar Awadallah, Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Palestina katika Umoja wa Mataifa na Taasisi zake Maalum na kueleza kuwa, utawala wa Kizayuni unaendelea kutekeleza sera zake za kibaguzi dhidi ya Wapalestina huku ukipuuza kanuni zote za kimataifa.

Ameiambia Radio ya Sauti ya Palestina kuwa, jukwaa hilo litawapa fursa Wapalestina kuwasilisha malalamiko yao kwa chombo hicho cha kisheria chenye makao makuu yake mjini Hague nchini Uholanzi kupitia njia ya kielektroniki.

Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Palestina katika Umoja wa Mataifa amesema kuna haja kwa jamii ya kimataifa kuendelea kuushinikiza utawala wa Kizayuni uachane na jinai zake za kila uchao dhidi ya Wapalestina.

Utawala wa Kizayuni unavyoua watoto wa Kipalestina

Jana Jumanne, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ilitoa mwito kwa ICC iharakishe mchakato wa kuuchunguza na kuuwajibisha utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na sera zake za kibaguzi na jinai za kutisha dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.

Hivi karibuni pia, Bunge la Palestina liliwasilisha kesi mbele ya ICC dhidi ya utawala vamizi wa Israel, kutokana na mzingiro wa Ukanda wa Gaza unaoendelea kwa miaka mingi. Limeitaka mahakama hiyo kuweka utaratibu wa kuiwajibisha Israel kwa uhalifu wake dhidi ya Ukanda wa Gaza na kutoa adhabu kali kwa mujibu wa kanuni za mahakama hiyo, mbali na kuwalipa fidia waathirika wa jinai hizo.

Tags