Putin apongeza uzinduzi wa 'kombora lenye nguvu zaidi duniani'
https://parstoday.ir/sw/news/world-i138338-putin_apongeza_uzinduzi_wa_'kombora_lenye_nguvu_zaidi_duniani'
Russia imefanya majaribio ya kombora jipya la balestiki lenye uwezo wa kupiga shabaha kutoka bara moja hadi jingine, huku Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo akilitaja kombora hilo lenye uwezo wa kutumia silaha za nyuklia kwa jina la "Sarmat" kuwa kombora "lenye nguvu zaidi" duniani.
(last modified 2026-05-14T03:27:00+00:00 )
May 14, 2026 03:24 UTC
  • Majaribio ya kombora
    Majaribio ya kombora "Shetani II"

Russia imefanya majaribio ya kombora jipya la balestiki lenye uwezo wa kupiga shabaha kutoka bara moja hadi jingine, huku Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo akilitaja kombora hilo lenye uwezo wa kutumia silaha za nyuklia kwa jina la "Sarmat" kuwa kombora "lenye nguvu zaidi" duniani.

Televisheni ya serikali imerusha video ya Kamanda Sergei Karakayev Mkuu wa Kikosi cha Kistratejia cha Makambora cha Russia akimtaarifu Rais Putin kuhusu kurushwa kwa mafanikio kombora hilo lenye nguvu kubwa zaidi duniani.

"Hili ndilo kombora lenye nguvu zaidi duniani," alisema Putin katika hotuba yake ya pongezi iliyorushwa kwa wananchi kwa njia ya televisheni.

Putin amesema Sarmat lina uwezo wa kuruka chini ya obiti, na kuipa masafa ya zaidi ya kilomita 35,000 (maili 21,750), na kudai linaweza "kupenya mifumo yote ya ulinzi dhidi ya makombora iliyopo na ya baadaye".

Russia ilianza kuunda kombora hilo mwaka 2011, na lilifaulu katika jaribio lake moja tu ambapo mwaka 2024 kombora hilo lililipuka wakati wa jaribio lake jingine.

Kombora la Sarmat ambalo huko Magharibi limepewa jina la "Shetani II", limekusudiwa kuchukua nafasi ya makombora 40 ya Voyevoda yaliyotengenezwa na utawala wa Usovieti.