Hujuma za chuki dhidi ya Uislamu zaongezeka Canada, Waislamu waonya
https://parstoday.ir/sw/news/world-i29492-hujuma_za_chuki_dhidi_ya_uislamu_zaongezeka_canada_waislamu_waonya
Taasisi ya Waislamu ya mjini Quebec nchini Canada imeonya juu ya ongezeko la vitendo vya chuki dhidi ya wafuasi wa dini hiyo mjini hapo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 24, 2017 02:19 UTC
  • Hujuma za chuki dhidi ya Uislamu zaongezeka Canada, Waislamu waonya

Taasisi ya Waislamu ya mjini Quebec nchini Canada imeonya juu ya ongezeko la vitendo vya chuki dhidi ya wafuasi wa dini hiyo mjini hapo.

Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo ya Waislamu, sambamba na kulaani kitendo cha kuweka mabango yenye jumbe za chuki dhidi ya Uislamu mjini Quebec, imesema kuwa, wakazi wa mji huo na Waislamu kwa ujumla watakabiliana na vitendo hivyo vya kibaguzi.

Watoto wa Kiislamu nchini Canada

Uenezwaji wa mabango hayo yenye jumbe za kibaguzi dhidi ya Waislamu katika kampeni za mgombea mmoja kwa ajili ya uchaguzi mdogo jimboni hapo, umeibua malalamiko na ukosoaji mkubwa kwa wakazi wa Quebec. Katika mabango hayo kuna picha ya kumdhalilisha mwanamke wa Kiislamu. Polisi ya eneo la Montreal la mji wa Quebec limeyaondoa mabango yote mjini hapo kufuatia malalamiko mengi yaliyowasilishwa katika siku za hivi karibuni. Hii ni katika hali ambayo, vitendo vya ubaguzi na chuki dhidi ya Waislamu nchini Canada vimeshtadi katika miezi ya hivi karibuni.

Shambulio la Canada mwanzoni mwa mwaka huu

Kwa akali watu watano waliuawa katika hujuma ya kikatili dhidi ya msikiti mmoja katika mji wa Quebec nchini Canada mwanzoni mwa mwaka huu. Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau alilaani shambulizi hilo dhidi ya msikiti na kulitaja kama hujuma ya kigaidi dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo.