Kimbunga cha Harvey chaua makumi ya watu Marekani
Kimbunga cha Harvey kinachoambatana na mafuriko kimeua makumi ya watu na kuwalazimisha wengine zaidi ya milioni moja kukimbia makazi yao nchini Marekani hussuan katika jimbo la Texas.
Kimbunga hicho kikali kumeharibu nyumba na miundombinu katika mingi mingi na ripoti zinasema baadhi ya miji ya Marekani kama Beaumont huko mashariki mwa Houston imepoteza kabisa taasisi za maji safi, wakati jeshi likiendelea kuokoa watu waliokumbwa na maafa hayo.
Wakazi karibu laki nane wa jimbo la Texas wametakiwa kuhama nyumba zao na wengine karibu milioni moja wamekimbia maskani na makazi yao wao wenyewe kwa kuhofia hatari ya mafuriko.
Maafisa wa serikali ya Marekani katika jimbo la Texas wanasema kuwa, watu wasiopungua 44 wamefariki dunia hadi sasa kutokana na kimbunga hicho na makumi ya wengine hawajulikani waliko.
Kimbunga cha Harvey katika mji wa nne kwa ukubwa nchini Marekani wa Houston kinasemekana kuwa hakijawahi kutokea katika jimbo la Texas katika kipindi cha zaidi ya miongo mitano iliyopita.
Maafisa wa jimbo la Texas wanasema kuwa, hasara iliyosababishwa na tufani ya Harvey katika jimbo hilo yumkini ikawa kubwa zaidi ya ile ya Katrina hapo mwaka 2005.