Nchi za Kiislamu zaafiki mpango wa UN wa kuwasaidia Waislamu Myanmar
https://parstoday.ir/sw/news/world-i34163-nchi_za_kiislamu_zaafiki_mpango_wa_un_wa_kuwasaidia_waislamu_myanmar
Nchi za Kiislamu duniani zimeafiki mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuwasaidia wakimbizi 300,000 Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar ambao wamekimbilia nchini jirani ya Bangladesh kuokoa maisha yao.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Sep 10, 2017 09:55 UTC
  • Nchi za Kiislamu zaafiki mpango wa UN wa kuwasaidia Waislamu Myanmar

Nchi za Kiislamu duniani zimeafiki mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuwasaidia wakimbizi 300,000 Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar ambao wamekimbilia nchini jirani ya Bangladesh kuokoa maisha yao.

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imeafiki mpango huo ambao umewasilishwa na Umoja wa Mataifa pamoja na taasisi kadhaa za kimataifa ambao unajumuisha kupelekea misaada ya dharura kwa wakimbizi laki tatu wa jamii ya Waislamu wa kabila la Rohingya walikimbilia hifadhi nchini Bangladesh kufuatia kuangamizwa kwa umati wenzao nchini Myanmar. Kati ya misaada hiyo ni vyakula, maji na dawa.

Hivi sasa taasisi kadhaa za Umoja wa Mataifa ziko katika maeneo ya mpakani kuwasaidia Waislamu wa kabila la Rohingya ambao wanazidi kumiminika katika nchi hiyo.

Hali nchini Myanmar

Tume ya Wakimbizi ya Umoja wa Maaifa UNHCR inasema katika kipindi cha wiki mbili zilizopita karibu Waislamu laki tatu wameingia Bangladesh wakikimbia mauaji ya kimbari Myanmar.

Taarifa zinasema tokea Agosti 25 wakati Jeshi la Myanmar lilipoanzisha hujuma dhidi ya Waislamu katika jimbo la Rakhine, Waislamu zaidi ya elfu sita wameuawa kwa umati na wengine elfu nane wamejeruhiwa.